Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




1 Mambo ya Nyakati 22:9 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

9 tazama, utapata mwana, atakayekuwa mtu wa amani; nami nitampa amani mbele ya adui zake pande zote; kwani jina lake litakuwa Sulemani, nami nitawapa Israeli amani na utulivu siku zake;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

9 Hata hivyo, utapata mwana, ambaye atatawala kwa amani kwa sababu nitampa amani na maadui zake wote wa jirani. Jina lake litakuwa Solomoni, kwa maana katika siku za utawala wake, atailetea Israeli amani na utulivu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

9 Hata hivyo, utapata mwana, ambaye atatawala kwa amani kwa sababu nitampa amani na maadui zake wote wa jirani. Jina lake litakuwa Solomoni, kwa maana katika siku za utawala wake, atailetea Israeli amani na utulivu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

9 Hata hivyo, utapata mwana, ambaye atatawala kwa amani kwa sababu nitampa amani na maadui zake wote wa jirani. Jina lake litakuwa Solomoni, kwa maana katika siku za utawala wake, atailetea Israeli amani na utulivu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

9 Lakini utakuwa na mwana ambaye atakuwa mtu wa amani na utulivu, nami nitampa utulivu mbele ya adui zake wote pande zote. Jina lake ataitwa Sulemani, nami nitawapa Israeli amani na utulivu wakati wa utawala wake.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

9 Lakini utakuwa na mwana ambaye atakuwa mtu wa amani na utulivu nami nitampa utulivu mbele ya adui zake wote pande zote. Jina lake ataitwa Sulemani, nami nitawapa Israeli amani na utulivu wakati wa utawala wake.

Tazama sura Nakili




1 Mambo ya Nyakati 22:9
24 Marejeleo ya Msalaba  

Nenda uingie ndani kwa mfalme Daudi, ukamwambie, Je! Hukuniapia mimi mjakazi wako, Ee mfalme, bwana wangu, kusema, Hakika yake Sulemani mwana wako atamiliki baada yangu, na kuketi katika kiti changu cha enzi? Mbona basi anamiliki Adonia?


Basi akasema, Wajua ya kwamba ufalme ulikuwa wangu, na Israeli wote wakaniwekea nyuso zao ili mimi nimiliki; lakini sasa ufalme umegeuka kuwa wake ndugu yangu; kwa maana ulikuwa wake kutoka kwa BWANA.


Na sasa, Ee BWANA, Mungu wangu, umenitawaza niwe mfalme mimi mtumwa wako badala ya Daudi baba yangu; nami ni mtoto mdogo tu; sijui jinsi inipasavyo kutoka wala kuingia.


Yuda na Israeli walikuwa wengi kama mchanga wa pwani kwa wingi, wakila, na kunywa, na kufurahi.


Kwani alikuwa akitawala nchi yote upande huu wa Mto, toka Tifsa mpaka Gaza, juu ya wafalme wote wa upande huu wa Mto; naye alikuwa na amani pande zake zote.


Yuda na Israeli wakakaa salama, kila mtu chini ya mzabibu wake na chini ya mtini wake, tokea Dani mpaka Beer-sheba, siku zote za Sulemani.


Ila leo BWANA, Mungu wangu, amenipa amani kila upande; hakuna adui, wala tukio baya.


Na ahimidiwe BWANA, aliyewapa watu wake Israeli kustarehe, vile vile kama yote aliyoyaahidi. Halikukosa kupatikana neno lolote katika ahadi yake njema, aliyoahidi kwa mkono wa Musa, mtumishi wake.


Hata itakuwa, siku zako zitakapotimia, uende kulala pamoja na baba zako, nitainua mzawa wako nyuma yako, atakayekuwa wa wana wako; nami nitauimarisha ufalme wake.


Je! Si BWANA, Mungu wenu, aliye pamoja nanyi? Na kuwapa amani pande zote? Kwa kuwa wenyeji wa nchi amewatia mkononi mwangu; nayo nchi imetiishwa mbele za BWANA, na mbele ya watu wake.


uliyemtimizia mtumishi wako Daudi, baba yangu, ahadi uliyomwahidi; naam, ulinena kwa kinywa chako, ukayatimiza kwa mkono wako, kama ilivyo leo.


Akitoa utulivu yeye, ni nani awezaye kuhukumia makosa? Akificha uso wake, ni nani awezaye kumtazama? Kama hufanyiwa taifa, au mtu mmoja, ni sawasawa;


Ee Mungu, mpe mfalme hukumu zako, Na mwana wa mfalme haki yako.


Haki na isitawi wakati wa maisha yake yote, Nayo amani iwepo, hadi mwezi utakapokoma.


BWANA, utatuamuria amani; maana ni wewe pia uliyetutendea kazi zetu zote.


Mimi naiumba nuru, na kulihuluku giza; mimi nafanya suluhu, na kuhuluku ubaya; Mimi ni BWANA, niyatendaye hayo yote.


Mimi nayaumba matunda ya midomo; Amani, amani, kwake yeye aliye mbali, na kwake yeye aliye karibu; asema BWANA; nami nitamponya.


Maana BWANA asema hivi, Tazama, nitamwelekezea amani kama mto, na utukufu wa mataifa kama kijito kifurikacho, nanyi mtapata kunyonya; mtabebwa; na juu ya magoti mtabembelezwa.


Utukufu wa mwisho wa nyumba hii utakuwa mkuu kuliko utukufu wake wa kwanza, asema BWANA wa majeshi; na katika mahali hapa nitawapa amani, asema BWANA wa majeshi.


Ndipo Gideoni akamjengea BWANA madhabahu hapo, akaiita jina lake, Yehova-Shalomu; hata hivi leo iko huko katika Ofra ya Waabiezeri.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo