Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Mambo ya Nyakati 22:19 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

19 Basi sasa jitieni moyo na nia kumtafuta BWANA, Mungu wenu; inukeni basi, mkamjengee BWANA Mungu mahali patakatifu, ili kulileta sanduku la Agano la BWANA, na vyombo vitakatifu vya Mungu, ndani ya nyumba itakayojengwa kwa ajili ya jina la BWANA.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

19 Sasa, mtumikieni Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, kwa nia na moyo wote. Shime basi! Mjengeeni Mwenyezi-Mungu mahali patakatifu ili sanduku la agano la Mwenyezi-Mungu pamoja na vyombo vyote vitakatifu vitumiwavyo katika ibada, viwekwe ndani ya nyumba iliyojengwa kwa ajili ya Mwenyezi-Mungu.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

19 Sasa, mtumikieni Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, kwa nia na moyo wote. Shime basi! Mjengeeni Mwenyezi-Mungu mahali patakatifu ili sanduku la agano la Mwenyezi-Mungu pamoja na vyombo vyote vitakatifu vitumiwavyo katika ibada, viwekwe ndani ya nyumba iliyojengwa kwa ajili ya Mwenyezi-Mungu.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

19 Sasa, mtumikieni Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, kwa nia na moyo wote. Shime basi! Mjengeeni Mwenyezi-Mungu mahali patakatifu ili sanduku la agano la Mwenyezi-Mungu pamoja na vyombo vyote vitakatifu vitumiwavyo katika ibada, viwekwe ndani ya nyumba iliyojengwa kwa ajili ya Mwenyezi-Mungu.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

19 Sasa itoeni mioyo yenu na nafsi zenu katika kumtafuta Mwenyezi Mungu, Mungu wenu. Anzeni kujenga Maskani ya Bwana Mwenyezi Mungu, ili mweze kulileta Sanduku la Agano la Mwenyezi Mungu na vyombo vitakatifu vya Mungu katika Hekalu litakalojengwa kwa ajili ya Jina la Mwenyezi Mungu.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

19 Sasa itoeni mioyo yenu na nafsi zenu katika kumtafuta bwana Mwenyezi Mungu wenu. Anzeni kujenga Maskani ya bwana Mwenyezi Mungu, ili mweze kulileta Sanduku la Agano la bwana na vyombo vitakatifu vya Mungu katika Hekalu litakalojengwa kwa ajili ya Jina la bwana.”

Tazama sura Nakili




1 Mambo ya Nyakati 22:19
24 Marejeleo ya Msalaba  

Wajua kuwa Daudi baba yangu hakuweza kujenga nyumba kwa jina la BWANA, Mungu wake, kwa sababu ya vita vilivyomzunguka pande zote, hata BWANA alipowatia watu chini ya nyayo zake.


Na humo sanduku hili nimelifanyizia mahali, ambalo ndani yake mna maagano ya BWANA, aliyoyafanya na baba zetu, hapo alipowatoa katika nchi ya Misri.


Makuhani wakalileta sanduku la Agano la BWANA hadi mahali pake, katika chumba cha ndani cha ile nyumba, patakatifu pa patakatifu, naam, chini ya mbawa za makerubi.


Jisifuni kwa jina lake takatifu; Na ufurahi moyo wao wamtafutao BWANA.


Mtafuteni BWANA na nguvu zake; Utafuteni uso wake siku zote.


ya dhahabu, ya fedha, na ya shaba, na ya chuma, hapana hesabu; basi inuka ushike kazi, naye BWANA na awe pamoja nawe.


Daudi akamwambia Sulemani mwanawe, Kwangu mimi nia yangu ilikuwa kujenga nyumba kwa ajili ya jina la BWANA, Mungu wangu.


Nawe, Sulemani mwanangu, mjue Mungu wa baba yako, ukamtumikie kwa moyo mkamilifu, na kwa nia ya kumkubali; kwa kuwa BWANA huchunguza mioyo yote, na kuyatambua mawazo yote ya fikira; ukimtafuta, atakuwa nawe; ukimwacha, atakutupa milele.


Yehoshafati akaogopa, akauelekeza uso wake amtafute BWANA; akatangaza watu wote kufunga katika Yuda yote.


Makuhani wakaliingiza sanduku la Agano la BWANA mahali pake katika chumba cha ndani cha nyumba, patakatifu pa patakatifu, yaani, chini ya mabawa ya makerubi.


Ndimo nilimoliweka hilo sanduku, ambalo ndani yake mna agano la BWANA, alilolifanya na wana wa Israeli.


Heri wazitiio shuhuda zake, Wamtafutao kwa moyo wote.


Toka mbinguni BWANA aliwachungulia wanadamu, Aone kama yuko mtu mwenye hekima, Amtafutaye Mungu.


Neno moja nimelitaka kwa BWANA, Nalo ndilo nitakalolitafuta, Nikae nyumbani mwa BWANA Siku zote za maisha yangu, Niutazame uzuri wa BWANA, Na kutafakari hekaluni mwake.


Nao na wanifanyie patakatifu; ili nipate kukaa kati yao.


Ondoka, uangaze; kwa kuwa nuru yako imekuja, Na utukufu wa BWANA umekuzukia.


Nanyi mtanitafuta na kuniona, mtakaponitafuta kwa moyo wenu wote.


Nikamwelekezea Bwana Mungu uso wangu, ili kusihi kwa maombi, na dua, pamoja na kufunga, na kuvaa nguo za magunia na majivu.


Basi sasa, BWANA wa majeshi asema hivi, Zitafakarini njia zenu.


Pandeni milimani, mkalete miti, mkaijenge nyumba; nami nitaifurahia, nami nitatukuzwa, asema BWANA.


Naye, alipofika na kuiona neema ya Mungu akafurahi, akawasihi wote waambatane na Bwana kwa moyo wote.


Basi sasa, mbona unakawia? Simama, ubatizwe, ukaoshwe dhambi zako, ukiliitia jina lake.


Lakini huko, kama mkimtafuta BWANA, Mungu wako, utampata, ukimtafuta kwa moyo wako wote, na roho yako yote.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo