1 Mambo ya Nyakati 22:14 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC14 Basi sasa, tazama, katika shida yangu, nimeiwekea akiba nyumba ya BWANA, talanta laki moja za dhahabu, na talanta milioni moja za fedha; na shaba na chuma isiyo na uzani; kwa vile zilivyo tele; miti tena na mawe nimeweka akiba, nawe utaweza kuongeza. Tazama suraMatoleo zaidiBiblia Habari Njema14 Kwa juhudi kubwa, nimeiwekea akiba nyumba ya Mwenyezi-Mungu, talanta 100,000 za dhahabu, talanta 1,000,000 za fedha na idadi isiyopimika ya shaba na chuma, kwani ni nyingi sana. Nimeandaa mbao na mawe tayari. Lakini huna budi kuongezea. Tazama suraBiblia Habari Njema - BHND14 Kwa juhudi kubwa, nimeiwekea akiba nyumba ya Mwenyezi-Mungu, talanta 100,000 za dhahabu, talanta 1,000,000 za fedha na idadi isiyopimika ya shaba na chuma, kwani ni nyingi sana. Nimeandaa mbao na mawe tayari. Lakini huna budi kuongezea. Tazama suraBiblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza14 Kwa juhudi kubwa, nimeiwekea akiba nyumba ya Mwenyezi-Mungu, talanta 100,000 za dhahabu, talanta 1,000,000 za fedha na idadi isiyopimika ya shaba na chuma, kwani ni nyingi sana. Nimeandaa mbao na mawe tayari. Lakini huna budi kuongezea. Tazama suraNeno: Bibilia Takatifu14 “Nimejitaabisha sana ili kupata mahitaji kwa ajili ya Hekalu la Mwenyezi Mungu: talanta elfu mia moja za dhahabu, talanta milioni moja za fedha, na kiasi kisichopimika cha shaba na chuma, pia mbao na mawe. Nawe unaweza kuviongeza. Tazama suraNeno: Maandiko Matakatifu14 “Nimejitaabisha sana ili kupata mahitaji kwa ajili ya Hekalu la bwana: talanta 100,000 za dhahabu, talanta 1,000,000 za fedha na kiasi kisichopimika cha shaba na chuma, pia mbao na mawe. Nawe waweza kuviongeza. Tazama sura |
Basi kwa uwezo wangu wote nimeiwekea akiba nyumba ya Mungu wangu, dhahabu kwa vitu vya dhahabu, na fedha kwa vitu vya fedha, na shaba kwa vitu vya shaba, na chuma kwa vitu vya chuma, na miti kwa vitu vya miti; vito vya shohamu, na vya kujazia, vito vya njumu, na vya rangi mbalimbali, na mawe ya thamani ya kila namna, na marumaru tele.