Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

1 Mambo ya Nyakati 20:5 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

5 Kulikuwa na vita tena na Wafilisti; na Elhanani, mwana wa Yairi akamwua Lahmi nduguye Goliathi, Mgiti, ambaye mti wa mkuki wake ulikuwa kama mti wa mfumaji.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

5 Kulitokea tena vita na Wafilisti. Naye Elhanani mwana wa Yairi alimuua Lahmi nduguye Goliathi, Mgiti, ambaye mpini wa mkuki wake, ulikuwa kama mti wa mfumaji.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

5 Kulitokea tena vita na Wafilisti. Naye Elhanani mwana wa Yairi alimuua Lahmi nduguye Goliathi, Mgiti, ambaye mpini wa mkuki wake, ulikuwa kama mti wa mfumaji.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

5 Kulitokea tena vita na Wafilisti. Naye Elhanani mwana wa Yairi alimuua Lahmi nduguye Goliathi, Mgiti, ambaye mpini wa mkuki wake, ulikuwa kama mti wa mfumaji.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

5 Katika vita vingine na Wafilisti, Elhanani mwana wa Yairi alimuua Lahmi nduguye Goliathi, Mgiti, ambaye mkuki wake ulikuwa na mpini kama mti wa mfumaji.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

5 Katika vita vingine na Wafilisti, Elhanani mwana wa Yairi alimuua Lahmi nduguye Goliathi, Mgiti, ambaye mkuki wake ulikuwa na mpini kama mti wa mfumaji.

Tazama sura Nakili

1 Mambo ya Nyakati 20:5
7 Marejeleo ya Msalaba  

Kulikuwa na vita tena na Wafilisti huko Gobu; na Elhanani, mwana wa Yairi, Mbethlehemi, alimwua Goliathi, Mgiti, ambaye mpini wa mkuki wake ulikuwa kama mpini wa mfuma nguo

Huyo akamwua Mmisri, mtu mrefu sana, aliyekuwa wa dhiraa tano urefu wake; na yule Mmisri alikuwa na mkuki kama mti wa mfumaji mkononi; lakini yeye akamshukia na gongo, akamnyakulia Mmisri mkuki mkononi, akamwua kwa mkuki wake mwenyewe.

Kulikuwa na vita tena huko Gathi; ambapo palikuwa na mtu mrefu sana, mwenye vidole vya mikono na miguu ishirini na vinne, kila mguu sita, na kila mkono sita; naye alizaliwa na Mrefai.

Ndipo akatoka shujaa katika kambi ya Wafilisti, aliyeitwa Goliathi, wa Gathi, ambaye urefu wake ulikuwa mikono sita na shibiri moja.

Na mpini wa mkuki wake ulikuwa kama mti wa mfumaji; na kichwa cha mkuki wake kilikuwa shekeli mia sita za chuma uzito wake; na mtu aliyemchukulia ngao yake akamtangulia.

Yule kuhani akasema, Upanga wa Goliathi, yule Mfilisti, uliyemwua katika bonde la Ela, tazama, upo hapa, umefungwa ndani ya nguo nyuma ya naivera; ukipenda kuuchukua, haya! Uchukue, maana hapa hapana mwingine ila huo tu. Daudi akasema, Hapana mwingine kama ule; haya! Nipe.

Naye akamwuliza BWANA kwa ajili yake, akampa vyakula, akampa na ule upanga wa Goliathi, Mfilisti.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo