Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Mambo ya Nyakati 2:21 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

21 Na baadaye Hesroni akamwingilia binti wa Makiri, babaye Gileadi; ambaye alimtwaa alipokuwa na umri wa miaka sitini; naye akamzalia Segubu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

21 Hesroni alipokuwa na umri wa miaka sitini, alimwoa binti Makiri, dada yake Gileadi. Huyo alimzalia mwana jina lake Segubu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

21 Hesroni alipokuwa na umri wa miaka sitini, alimwoa binti Makiri, dada yake Gileadi. Huyo alimzalia mwana jina lake Segubu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

21 Hesroni alipokuwa na umri wa miaka sitini, alimwoa binti Makiri, dada yake Gileadi. Huyo alimzalia mwana jina lake Segubu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

21 Hatimaye, Hesroni alipokuwa na umri wa miaka sitini, alimwoa binti Makiri, babaye Gileadi. Akakutana kimwili naye, akamzalia Segubu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

21 Hatimaye, Hesroni akakutana kimwili na binti wa Makiri babaye Gileadi (ambaye alimwoa alipokuwa na umri wa miaka sitini), naye akamzaa Segubu.

Tazama sura Nakili




1 Mambo ya Nyakati 2:21
9 Marejeleo ya Msalaba  

Yusufu akaona wana wa Efraimu hata kizazi cha tatu; na wana wa Makiri, mwana wa Manase, walizaliwa magotini mwa Yusufu.


Naye Huri akamzaa Uri; na Uri akamzaa Besaleli.


Na Segubu akamzaa Yairi, aliyekuwa mwenye miji ishirini na mitatu katika nchi ya Gileadi.


Wana wa Manase; Asrieli, ambaye suria yake, Mwarami, alimzalia, akamzalia na Makiri babaye Gileadi;


Wana wa Manase; wa Makiri, jamaa ya Wamakiri; na Makiri akamzaa Gileadi; wa Gileadi, jamaa ya Wagileadi.


Wakati huo wakakaribia hao binti za Selofehadi, mwana wa Heferi, mwana wa Gileadi, mwana wa Makiri, mwana wa Manase, wa jamaa za Manase mwana wa Yusufu; na majina ya hao binti za Selofehadi ni haya; Mala, na Nuhu, na Hogla, na Milka, na Tirza.


Kisha Yairi mwana wa Manase akaenda na kuvitwaa vijiji vya Gileadi. Akaviita jina lake Hawoth-yairi.


Na Makiri nilimpa Gileadi.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo