Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Mambo ya Nyakati 19:3 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

3 Lakini wakuu wa wana wa Amoni wakamwambia Hanuni, Je! Unadhani Daudi amewatuma wafariji kwako kwa heshima ya baba yako? Je! Hawakukujia watumishi wake ili kuichunguza nchi, na kuiangamiza, na kuipeleleza?

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

3 Lakini viongozi wa Waamoni wakamwambia mfalme, “Je! Unadhani ni kwa sababu ya heshima ya baba yako ati Daudi ametuma wajumbe hawa waje kukufariji? Watu hawa si majasusi waliotumwa kuja kuichunguza nchi kuiangamiza na kuipeleleza?”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

3 Lakini viongozi wa Waamoni wakamwambia mfalme, “Je! Unadhani ni kwa sababu ya heshima ya baba yako ati Daudi ametuma wajumbe hawa waje kukufariji? Watu hawa si majasusi waliotumwa kuja kuichunguza nchi kuiangamiza na kuipeleleza?”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

3 Lakini viongozi wa Waamoni wakamwambia mfalme, “Je! unadhani ni kwa sababu ya heshima ya baba yako ati Daudi ametuma wajumbe hawa waje kukufariji? Watu hawa si majasusi waliotumwa kuja kuichunguza nchi kuiangamiza na kuipeleleza?”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

3 wakuu wa Waamoni wakamwambia Hanuni, “Hivi unadhani Daudi anamheshimu baba yako kwa kuwatuma wajumbe kukufariji? Je, hawa watu hawakuja kuipeleleza na kuidadisi nchi ili waishinde?”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

3 wakuu wa Waamoni wakamwambia Hanuni, “Hivi unadhani Daudi anamheshimu baba yako kwa kuwatuma wajumbe kukufariji? Je, hawa watu hawakuja kuipeleleza na kuidadisi nchi ili waishinde?”

Tazama sura Nakili




1 Mambo ya Nyakati 19:3
12 Marejeleo ya Msalaba  

Lakini wakuu wa Waamoni wakamwambia Hanuni, bwana wao, Je! Waona ya kuwa Daudi amemheshimu babayo kwa kutuma kwako wafariji? Je! Daudi hakuwapeleka watumishi wake kwako ili kuuangalia mji, na kuupeleleza, na kuuangamiza?


Naye Daudi akasema, Nitamtendea wema Hanuni, mwana wa Nahashi, kwa kuwa babaye alinitendea mimi wema. Basi Daudi akatuma wajumbe ili kumtuliza kwa habari za babaye. Wakaja watumishi wa Daudi katika nchi ya wana wa Amoni kwa Hanuni, ili wamtulize.


Basi Hanuni akawatwaa watumishi wa Daudi, akawanyoa, akawapasulia nguo zao katikati, hadi kiunoni, kisha akawaachilia waondoke.


Basi wana wa Dani wakatuma watu watano kutoka kwa koo zao zote, watu mashujaa, kutoka Sora, na kutoka Eshtaoli, ili kuipeleleza hiyo nchi, kuikagua; wakawaambia, Haya, endeni mkaikague nchi hii; basi wakaifikia nchi ya vilima vilima ya Efraimu, hadi nyumba ya huyo Mika, Wakalala huko.


Lakini wakuu wa Wafilisti wakamkasirikia, na kumwambia, Mrudishe huyu, apate kurejea mahali pake ulipomwagiza, wala asiende pamoja nasi vitani, asije akawa adui wetu vitani; kwani mtu huyu angejipatanisha na bwana wake kwa njia gani? Je! Si kwa vichwa vya watu hawa?


Akishi akajibu, akamwambia Daudi, Mimi najua ya kuwa u mwema machoni pangu, kama malaika wa Mungu; ila hao wakuu wa Wafilisti wamesema, Huyu hatakwea pamoja nasi kwenda vitani.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo