Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Mambo ya Nyakati 19:19 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

19 Na watumishi wa Hadadezeri walipojiona kuwa wameshindwa mbele ya Israeli, walifanya amani na Daudi, wakamtumikia; wala Washami hawakukubali kuwasaidia wana wa Amoni tena.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

19 Kisha watumishi wa Hadadezeri walipoona kuwa wameshindwa na Waisraeli, walifanya mapatano ya amani na Daudi nao wakawa watumishi wa Daudi. Hivyo Waaramu hawakukubali kuwasaidia Waamoni tena.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

19 Kisha watumishi wa Hadadezeri walipoona kuwa wameshindwa na Waisraeli, walifanya mapatano ya amani na Daudi nao wakawa watumishi wa Daudi. Hivyo Waaramu hawakukubali kuwasaidia Waamoni tena.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

19 Kisha watumishi wa Hadadezeri walipoona kuwa wameshindwa na Waisraeli, walifanya mapatano ya amani na Daudi nao wakawa watumishi wa Daudi. Hivyo Waaramu hawakukubali kuwasaidia Waamoni tena.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

19 Raia wa Hadadezeri walipoona kuwa wameshindwa na Israeli, wakafanya mapatano ya amani na Daudi, wakawa watumishi wake. Hivyo Waaramu hawakukubali kuwasaidia Waamoni tena.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

19 Raiya wa Hadadezeri walipoona kuwa wameshindwa na Israeli, wakafanya mapatano ya amani na Daudi, wakawa watumishi wake. Hivyo Waaramu hawakukubali kuwasaidia Waamoni tena.

Tazama sura Nakili




1 Mambo ya Nyakati 19:19
13 Marejeleo ya Msalaba  

Ikawa baadaye, mfalme wa Waamoni akafa, mwanawe Hanuni, akawa mfalme, badala yake.


Na wafalme wote waliomtumikia Hadadezeri walipojiona kuwa wameshindwa mbele ya Israeli, walifanya amani na Israeli, wakawatumikia. Basi Washami wakaogopa kuwasaidia Waamoni tena.


Basi, Ben-hadadi mfalme wa Aramu akakusanya jeshi lake lote; nao walikuwapo wafalme thelathini na wawili pamoja naye, na farasi, na magari: akakwea akauhusuru Samaria, akaupiga vita.


Ikawa, Ben-hadadi alipolisikia neno hilo, naye alikuwa akinywa, yeye na wafalme, mabandani, aliwaambia watumwa wake, Jipangeni. Wakajipanga juu ya mji.


Sifa za Daudi zikafika nchi zote; naye BWANA akawaletea mataifa yote hofu yake.


Washami wakakimbia mbele ya Israeli; naye Daudi akawaua katika Washami watu wa magari elfu saba, na askari waendao kwa miguu elfu arubaini, akamwua na Shobaki, jemadari wa jeshi.


Hata ikawa, mwanzo wa mwaka mpya, wakati watokapo wafalme kwenda vitani, Yoabu akawaongoza mashujaa wa jeshi, akaiteka nyara nchi ya wana wa Amoni, akaja akauzingira Raba. Lakini Daudi akakaa Yerusalemu. Naye Yoabu akaupiga Raba akauangamiza.


Nawe umenipa nguvu za vita, Hunitiishia chini yangu walionishambulia.


Mara tu waliposikia habari zangu, wakanitii. Wageni walinijia wakinyenyekea.


Maana asema, Je! Wakuu wangu si wote wafalme?


Tufuate:

Matangazo


Matangazo