Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Mambo ya Nyakati 19:18 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

18 Washami wakakimbia mbele ya Israeli; naye Daudi akawaua katika Washami watu wa magari elfu saba, na askari waendao kwa miguu elfu arubaini, akamwua na Shobaki, jemadari wa jeshi.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

18 Lakini Waaramu walikimbia mbele ya Waisraeli. Daudi aliwaua Waaramu waendeshao magari 7,000 na askari wa miguu 40,000. Pia alimuua Shofaki, kamanda wa jeshi lao.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

18 Lakini Waaramu walikimbia mbele ya Waisraeli. Daudi aliwaua Waaramu waendeshao magari 7,000 na askari wa miguu 40,000. Pia alimuua Shofaki, kamanda wa jeshi lao.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

18 Lakini Waaramu walikimbia mbele ya Waisraeli. Daudi aliwaua Waaramu waendeshao magari 7,000 na askari wa miguu 40,000. Pia alimuua Shofaki, kamanda wa jeshi lao.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

18 Lakini Waaramu wakakimbia mbele ya Israeli, naye Daudi akawaua waendesha magari ya vita elfu saba, na askari wa miguu elfu arobaini. Pia akamuua Shofaki, jemadari wa jeshi lao.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

18 Lakini Waaramu wakakimbia mbele ya Israeli, naye Daudi akawaua waendesha magari 7,000 na askari wao wa miguu 40,000. Pia akamuua Shofaki, jemadari wa jeshi lao.

Tazama sura Nakili




1 Mambo ya Nyakati 19:18
7 Marejeleo ya Msalaba  

Wakakimbia Washami mbele ya Israeli; naye Daudi akawaua katika Washami, watu wa magari mia saba, na wapanda farasi elfu arubaini, naye akampiga huyo Shobaki, jemadari wa jeshi lao, hata akafa huko.


Alipoambiwa Daudi; akakusanya Israeli wote, akavuka Yordani, akawajia, akapanga vita juu yao. Basi Daudi alipopanga vita juu ya Washami, wakapigana naye.


Na watumishi wa Hadadezeri walipojiona kuwa wameshindwa mbele ya Israeli, walifanya amani na Daudi, wakamtumikia; wala Washami hawakukubali kuwasaidia wana wa Amoni tena.


Mungu ndiye anifungaye mshipi wa nguvu, Naye anaifanya kamilifu njia yangu.


Mfalme haokolewi kwa jeshi lake kubwa, Wala shujaa haokoki kwa kuwa na nguvu nyingi.


BWANA wa majeshi yu pamoja nasi, Mungu wa Yakobo ni kimbilio letu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo