Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Mambo ya Nyakati 19:16 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

16 Na Washami walipojiona kuwa wameshindwa mbele ya Israeli, wakatuma wajumbe, wakawaleta Washami walioko ng'ambo ya Mto, na Shobaki, jemadari wa jeshi la Hadadezeri, akawaongoza.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

16 Lakini Waaramu walipoona ya kwamba wameshindwa na Waisraeli, walituma wajumbe waende kuwaleta Waaramu wengine waliokuwa ngambo ya mto Eufrate wakiongozwa na Shofaki, kamanda wa jeshi la Hadadezeri.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

16 Lakini Waaramu walipoona ya kwamba wameshindwa na Waisraeli, walituma wajumbe waende kuwaleta Waaramu wengine waliokuwa ngambo ya mto Eufrate wakiongozwa na Shofaki, kamanda wa jeshi la Hadadezeri.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

16 Lakini Waaramu walipoona ya kwamba wameshindwa na Waisraeli, walituma wajumbe waende kuwaleta Waaramu wengine waliokuwa ng'ambo ya mto Eufrate wakiongozwa na Shofaki, kamanda wa jeshi la Hadadezeri.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

16 Baada ya Waaramu kuona kwamba wameshindwa na Israeli, wakapeleka wajumbe na kuwataka Waaramu wengine kutoka ng’ambo ya Mto, wakiongozwa na Shofaki, jemadari wa jeshi la Hadadezeri.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

16 Baada ya Waaramu kuona kwamba wameshindwa na Israeli, wakapeleka wajumbe na kuwataka Waaramu wengine kutoka ng’ambo ya Mto Frati, wakiongozwa na Shofaki, jemadari wa jeshi la Hadadezeri.

Tazama sura Nakili




1 Mambo ya Nyakati 19:16
7 Marejeleo ya Msalaba  

Naye Hadadezeri akatuma na kuwaleta Washami waliokuwako ng'ambo ya Mto; nao wakaja Helamu, naye Shobaki, jemadari wa jeshi la Hadadezeri, akawaongoza.


Na wana wa Amoni walipoona ya kwamba Washami wamekimbia, wakakimbia nao mbele ya Abishai, nduguye, wakaingia mjini. Ndipo Yoabu akaja Yerusalemu.


Alipoambiwa Daudi; akakusanya Israeli wote, akavuka Yordani, akawajia, akapanga vita juu yao. Basi Daudi alipopanga vita juu ya Washami, wakapigana naye.


Mbona mataifa yanafanya ghasia, Na watu kuwaza mambo ya bure?


Ungameni pamoja, enyi makabila ya watu, Nanyi mtavunjwa vipande vipande; Tegeni masikio, ninyi nyote wa nchi zilizo mbali; Jitahidini, nanyi mtavunjwa vipande vipande; Jitahidini, nanyi mtavunjwa vipande vipande.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo