Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Mambo ya Nyakati 18:4 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

4 Daudi akampokonya magari elfu moja, na wapanda farasi elfu saba, na askari waendao kwa miguu elfu ishirini; Daudi akawakata mshipa farasi wote wa magari, ila wa magari mia moja akawaweka.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

4 Daudi akateka magari ya farasi 1,000, askari wapandafarasi 7,000 na wa miguu 20,000. Kisha Daudi alikata mishipa ya miguu ya nyuma ya farasi wote wa magari, ila aliwabakiza 100.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

4 Daudi akateka magari ya farasi 1,000, askari wapandafarasi 7,000 na wa miguu 20,000. Kisha Daudi alikata mishipa ya miguu ya nyuma ya farasi wote wa magari, ila aliwabakiza 100.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

4 Daudi akateka magari ya farasi 1,000, askari wapandafarasi 7,000 na wa miguu 20,000. Kisha Daudi alikata mishipa ya miguu ya nyuma ya farasi wote wa magari, ila aliwabakiza 100.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

4 Daudi akateka magari ya vita elfu moja miongoni mwa magari yake, waendesha hayo magari ya vita elfu saba, na askari wa miguu elfu ishirini. Daudi akakata mishipa ya miguu ya farasi wa magari ya vita, akabakiza farasi mia moja.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

4 Daudi akateka magari ya vita 1,000 miongoni mwa magari yake, waendesha hayo magari ya kukokotwa na farasi 7,000 na askari wa miguu 20,000. Daudi akakata mishipa ya miguu ya nyuma ya farasi wote wakokotao magari, ila akabakiza 100.

Tazama sura Nakili




1 Mambo ya Nyakati 18:4
11 Marejeleo ya Msalaba  

Nafsi yangu, usiingie katika siri yao, Fahari yangu usiungane na kusanyiko lao, Maana katika ghadhabu yao walimwua mtu, Na kwa ukaidi wao walikata mshipa wa ng'ombe;


Daudi akampokonya wapanda farasi elfu moja na mia saba na askari waliokwenda kwa miguu elfu ishirini; Daudi akawakata mshipa farasi wote wa magari, ila farasi wa magari mia moja akawabakiza.


Sulemani akakusanya magari na wapandao farasi; naye alikuwa na magari elfu moja mia nne, na wapandao farasi elfu kumi na mbili, aliowaweka katika miji ya magari, na pamoja na mfalme huko Yerusalemu.


Na hawa ndio wakuu aliokuwa nao; Azaria mwana wa Sadoki, kuhani,


Tena Daudi akampiga Hadadezeri, mfalme wa Soba, mpaka Hamathi, alipokwenda kujisimamishia mnara wa ukumbusho kwenye mto wa Frati.


Na Washami wa Dameski walipokuja wamsaidie Hadadezeri, mfalme wa Soba, Daudi akapiga katika hao Washami watu elfu ishirini na mbili.


Hawa wanataja magari na hawa farasi, Lakini sisi tutalitaja jina la BWANA, Mungu wetu.


Ila asifanye farasi wake kuwa wengi, wala asiwarudishe watu Misri, ili apate kufanya farasi kuwa wengi; kwa kuwa BWANA amewaambia, Tangu sasa msirudie tena njia ile.


BWANA akamwambia Yoshua, Wewe usiogope kwa ajili ya hao; kwani kesho wakati kama huu nitawatoa wakiwa wameuawa wote mbele ya Israeli; utawakata farasi wao, na magari yao utayateketeza kwa moto.


Yoshua akawafanyia vile vile kama BWANA alivyomwamuru; akawakata farasi wao, na kuteketeza magari yao kwa moto.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo