Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Mambo ya Nyakati 18:2 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

2 Akapiga Moabu; na hao Wamoabi wakawa watumishi wa Daudi wakaleta zawadi.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

2 Aliwashinda Wamoabu pia, wakawa watumishi wake na wakawa wanalipa kodi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

2 Aliwashinda Wamoabu pia, wakawa watumishi wake na wakawa wanalipa kodi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

2 Aliwashinda Wamoabu pia, wakawa watumishi wake na wakawa wanalipa kodi.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

2 Pia Daudi akawashinda Wamoabu, wakawa watumishi wake, nao wakawa wanamletea ushuru.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

2 Pia Daudi akawashinda Wamoabu, wakawa watumishi wake, nao wakawa wanamletea ushuru.

Tazama sura Nakili




1 Mambo ya Nyakati 18:2
14 Marejeleo ya Msalaba  

Akapiga Moabu, akawapima kwa kamba wakiwa wamelazwa chini; akapima kamba mbili za kuuawa, na kamba moja nzima ya kuhifadhi hai. Wamoabi wakawa watumishi wa Daudi, wakaleta zawadi.


Akaingia Yerusalemu na wafuasi wengi sana, na ngamia wachukuao manukato, na dhahabu nyingi sana, na vito vya thamani; alipomfikia Sulemani, akazungumza naye mambo yote aliyokuwa nayo moyoni.


Wakaleta kila mtu zawadi yake, vyombo vya fedha, na vyombo vya dhahabu, na mavazi, na silaha, na manukato, na farasi, na nyumbu, hesabu yake ya mwaka kwa mwaka.


Ikawa baadaye, Daudi akawapiga Wafilisti, akawashinda, akautwaa Gathi na vijiji vyake mikononi mwa Wafilisti.


Tena Daudi akampiga Hadadezeri, mfalme wa Soba, mpaka Hamathi, alipokwenda kujisimamishia mnara wa ukumbusho kwenye mto wa Frati.


Moabu ni bakuli langu la kunawia. Nitamtupia Edomu kiatu changu, Na kumpigia Filisti kelele za vita.


Nao watashuka, watalirukia bega la Wafilisti upande wa magharibi; nao pamoja watawateka wana wa mashariki; watanyosha mkono juu ya Edomu na Moabu; na wana wa Amoni watawatii.


Pelekeni wana-kondoo, kodi yake aitawalaye nchi toka Sela kuelekea jangwani, mpaka mlima wa binti Sayuni.


Namwona, lakini si sasa; Namtazama, lakini si karibu; Nyota itatokea katika Yakobo Na fimbo ya enzi itainuka katika Israeli; Nayo itazipigapiga pembe za Moabu, Na kuwavunjavunja wana wote wa ghasia.


Lakini wengine wasiofaa kitu wakasema, Huyu je! Atatuokoaje? Nao wakamdharau, wasimletee zawadi.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo