Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Mambo ya Nyakati 17:6 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

6 Katika mahali kote nilikokwenda na Israeli wote, je! Nimesema neno lolote na mtu yeyote wa waamuzi wa Israeli, niliowaagiza kuwalisha watu wangu, nikisema, Mbona hamkunijengea nyumba ya mwerezi?

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

6 Je, kila mahali ambako nimekwenda na Waisraeli, nimepata kumwuliza mwamuzi wao yeyote niliyemwamuru awachunge watu wangu, “Kwa nini hukunijengea nyumba ya mierezi?” ’

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

6 Je, kila mahali ambako nimekwenda na Waisraeli, nimepata kumwuliza mwamuzi wao yeyote niliyemwamuru awachunge watu wangu, “Kwa nini hukunijengea nyumba ya mierezi?” ’

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

6 Je, kila mahali ambako nimekwenda na Waisraeli, nimepata kumwuliza mwamuzi wao yeyote niliyemwamuru awachunge watu wangu, “Kwa nini hukunijengea nyumba ya mierezi?”’

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

6 Popote nilipoenda pamoja na Waisraeli wote, je, kuna wakati nilimuuliza kiongozi yeyote niliyemwagiza kuwachunga watu wangu, “Kwa nini hujanijengea nyumba ya mwerezi?” ’

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

6 Je, popote nilipokwenda pamoja na Waisraeli wote, wakati wowote nilimwambia kiongozi yeyote niliyemwagiza kuwachunga watu wangu, kwa nini hujanijengea nyumba ya mierezi?’ 

Tazama sura Nakili




1 Mambo ya Nyakati 17:6
19 Marejeleo ya Msalaba  

Mahali kote nilikokwenda na wana wa Israeli wote, je! Nimesema neno lolote na mtu yeyote wa waamuzi wa Israeli, niliyemwagiza kuwalisha watu wangu Israeli, nikisema, Mbona hamkunijengea nyumba ya mierezi?


Tokea siku ile nilipowatoa watu wangu Israeli katika Misri, sikuchagua mji wowote katika kabila zote za Israeli ili kujenga nyumba, jina langu liwe hapo; lakini nilimchagua Daudi awe juu ya watu wangu Israeli.


Katika zamani za kale, hata hapo Sauli alipokuwa mfalme, wewe ndiwe uliyeongoza jeshi la Israeli. Naye BWANA, Mungu wako, akakuambia, Ndiwe, utakayewalisha watu wangu Israeli, ndiwe utakayekuwa mkuu juu ya watu wangu Israeli.


Basi sasa ndivyo utakavyomwambia mtumishi wangu Daudi, BWANA wa majeshi asema hivi, Nilikutwaa kutoka machungani, hata katika kuwafuata kondoo ili uwe mkuu juu ya watu wangu Israeli;


Nami nitaweka juu yao wachungaji watakaowalisha; wala hawataona hofu tena, wala kufadhaika, wala hatapotea hata mmoja wao, asema BWANA.


Mwanadamu, toa unabii juu ya wachungaji wa Israeli, toa unabii, uwaambie, naam, hao wachungaji, Bwana MUNGU asema hivi; Ole wao wachungaji wa Israeli, wanaojilisha wenyewe; je! Haiwapasi wachungaji kuwalisha kondoo?


Naye atasimama, na kulisha kundi lake kwa nguvu za BWANA, kwa enzi ya jina la BWANA, Mungu wake; nao watakaa; maana sasa atakuwa mkuu hadi miisho ya dunia.


Nawe Bethlehemu, katika nchi ya Yuda, Hu mdogo kamwe miongoni mwa watawala wa Yuda; Kwa kuwa kwako atatoka mtawala Atakayewachunga watu wangu Israeli.


baada ya hayo akawapa waamuzi hata wakati wa nabii Samweli.


Tena pana mapatano gani kati ya hekalu la Mungu na sanamu? Kwa maana sisi tu hekalu la Mungu aliye hai; kama Mungu alivyosema, ya kwamba, Nitakaa ndani yao, na kati yao nitatembea, nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.


kwa kuwa BWANA. Mungu wako, yuatembea katika kituo akuokoe, na kukutolea adui zako mbele yako; kwa hiyo na kiwe kitakatifu kituo chako; asije akaona kitu kwako kisichokuwa safi, akageuka na kukuacha.


Kwa malaika wa kanisa lililoko Efeso andika; Haya ndiyo anenayo yeye azishikaye hizo nyota saba katika mkono wake wa kulia, yeye aendaye katikati ya vile vinara saba vya dhahabu.


BWANA akawatuma Yerubaali, na Baraka, na Yeftha, na Samweli, akawaokoa ninyi kutoka kwa mikono ya adui zenu pande zote, nanyi mkakaa salama.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo