Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Mambo ya Nyakati 17:24 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

24 Jina lako na liwe imara, likatukuzwe milele, kusema, BWANA wa majeshi ndiye Mungu wa Israeli, naam, Mungu juu ya Israeli; na hiyo nyumba ya Daudi mtumwa wako imefanywa imara mbele zako.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

24 Nalo jina lako litatukuzwa milele, nao watu watasema, ‘Mwenyezi-Mungu wa majeshi, Mungu wa Israeli, ndiye Mungu wa Israeli!’ Na jamaa yangu, mimi Daudi mtumishi wako, itaimarika mbele yako.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

24 Nalo jina lako litatukuzwa milele, nao watu watasema, ‘Mwenyezi-Mungu wa majeshi, Mungu wa Israeli, ndiye Mungu wa Israeli!’ Na jamaa yangu, mimi Daudi mtumishi wako, itaimarika mbele yako.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

24 Nalo jina lako litatukuzwa milele, nao watu watasema, ‘Mwenyezi-Mungu wa majeshi, Mungu wa Israeli, ndiye Mungu wa Israeli!’ Na jamaa yangu, mimi Daudi mtumishi wako, itaimarika mbele yako.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

24 ili ithibitike na jina lako litakuwa kuu milele. Kisha watu watasema, ‘Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, Mungu aliye juu ya Israeli, ndiye Mungu wa Israeli.’ Nayo nyumba ya mtumishi wako Daudi itafanywa imara mbele zako.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

24 ili ithibitike na jina lako litakuwa kuu milele. Kisha watu watasema, ‘bwana Mungu Mwenye Nguvu Zote, Mungu aliye juu ya Israeli, ndiye Mungu wa Israeli.’ Nayo nyumba ya mtumishi wako Daudi itafanywa imara mbele zako.

Tazama sura Nakili




1 Mambo ya Nyakati 17:24
17 Marejeleo ya Msalaba  

Basi sasa, Ee BWANA, neno lile ulilolinena kuhusu mtumishi wako, na kuhusu nyumba yake, na lifanywe imara milele, ukafanye kama ulivyosema.


Kwa kuwa wewe, Ee Mungu wangu, umenifunulia mimi mtumishi wako ya kuwa utanijengea nyumba; kwa hiyo mimi mtumishi wako nimeona vema moyoni mwangu kuomba mbele yako.


basi usikie huko mbinguni, toka makaoni mwako, ukatende yote atakayokuomba huyo mgeni; ili watu wote wa dunia wapate kulijua jina lako, na kukucha wewe, kama watu wako Israeli, tena wajue ya kuwa nyumba hii niliyoijenga imeitwa kwa jina lako.


Ee BWANA, utukuzwe kwa nguvu zako, Nasi tutaimba na kuuhimidi uwezo wako.


Jina lake tukufu na lihimidiwe milele; Dunia yote na ijae utukufu wake. Amina na Amina.


Na fadhili za BWANA, Mungu wetu, ziwe juu yetu, Na kazi ya mikono yetu uifanye thabiti, Naam, kazi ya mikono yetu uifanikishe.


Wakati huo, asema BWANA, nitakuwa Mungu wa jamaa zote za Israeli, nao watakuwa watu wangu.


Ndipo Yeremia akamwambia Sedekia, BWANA, Mungu wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Kama ukitoka kwenda kwa wakuu wa mfalme wa Babeli, basi nafsi yako utaishi, wala mji huu hautateketezwa; nawe utaishi na nyumba yako;


Na usitutie majaribuni, lakini utuokoe na yule mwovu. [Kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu, na utukufu, hata milele. Amina.]


Basi ninyi salini hivi; Baba yetu uliye mbinguni, Jina lako litukuzwe, Ufalme wako uje,


Baba, ulitukuze jina lako. Basi ikaja sauti kutoka mbinguni, Nimelitukuza, nami nitalitukuza tena.


Maneno hayo aliyasema Yesu; akainua macho yake kuelekea mbinguni, akasema, Baba, saa imekwisha kufika. Mtukuze Mwanao, ili Mwana wako naye akutukuze wewe;


na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI BWANA, kwa utukufu wa Mungu Baba.


Lakini sasa wanaitamani nchi iliyo bora, yaani, ya mbinguni. Kwa hiyo Mungu haoni haya kuitwa Mungu wao; maana amewatengenezea mji.


Maana hili ndilo agano nitakaloagana na nyumba ya Israeli Baada ya siku zile, asema Bwana; Nitawapa sheria zangu katika fikira zao, Na katika mioyo yao nitaziandika; Nami nitakuwa Mungu kwao, Nao watakuwa watu wangu.


Mtu akisema, na aseme kama asemaye maneno halisi ya Mungu; mtu akihudumu, na ahudumu kwa nguvu anazojaliwa na Mungu; ili Mungu atukuzwe katika mambo yote kwa Yesu Kristo. Utukufu na uweza una yeye hata milele na milele. Amina.


Nikasikia sauti kubwa kutoka katika kile kiti cha enzi ikisema, Tazama, maskani ya Mungu ni pamoja na wanadamu, naye atafanya maskani yake pamoja nao, nao watakuwa watu wake. Naye Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo