Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Mambo ya Nyakati 17:2 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

2 Naye Nathani akamwambia Daudi, Haya, fanya yote yaliyomo moyoni mwako; kwa maana Mungu yu pamoja nawe.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

2 Nathani akamwambia Daudi, “Fanya chochote unachofikiria moyoni mwako, kwa kuwa Mungu yu pamoja nawe.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

2 Nathani akamwambia Daudi, “Fanya chochote unachofikiria moyoni mwako, kwa kuwa Mungu yu pamoja nawe.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

2 Nathani akamwambia Daudi, “Fanya chochote unachofikiria moyoni mwako, kwa kuwa Mungu yu pamoja nawe.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

2 Nathani akamjibu Daudi, “Lolote ulilo nalo moyoni mwako litende, kwa maana Mungu yu pamoja nawe.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

2 Nathani akamjibu Daudi, “Lolote ulilo nalo moyoni mwako litende, kwa maana Mungu yu pamoja nawe.”

Tazama sura Nakili




1 Mambo ya Nyakati 17:2
13 Marejeleo ya Msalaba  

Nathani akamwambia mfalme, Haya, fanya yote yaliyomo moyoni mwako; maana BWANA yuko pamoja nawe.


Basi ilikuwa moyoni mwake Daudi, baba yangu, kujenga nyumba kwa jina la BWANA, Mungu wa Israeli.


Ikawa, Daudi alipokuwa akikaa nyumbani mwake, Daudi akamwambia nabii Nathani, Angalia, mimi ninakaa katika nyumba ya mwerezi, bali sanduku la Agano la BWANA linakaa chini ya mapazia.


Ikawa usiku uo huo, neno la Mungu likamjia Nathani, kusema,


Daudi akamwambia Sulemani mwanawe, Kwangu mimi nia yangu ilikuwa kujenga nyumba kwa ajili ya jina la BWANA, Mungu wangu.


Ndipo Daudi mfalme akasimama kwa miguu yake, akasema, Nisikilizeni, ndugu zangu, na watu wangu; Mimi nilikuwa na nia ya kuijenga nyumba ya kuliweka sanduku la Agano la BWANA, na kiti cha kuwekea miguu cha Mungu wetu; hata nilikuwa nimejitayarisha kujenga.


Akujalie kwa kadiri ya haja ya moyo wako, Na kukutimizia mipango yako yote.


BWANA wa majeshi asema hivi, Siku hizo watu kumi, wa lugha zote za mataifa, wataushika upindo wa nguo yake yeye aliye Myahudi; naam, wataushika wakisema, Tutakwenda pamoja nanyi, kwa maana tumesikia kwamba Mungu yuko pamoja nanyi.


Akaingia nyumbani kwake akasema, Salamu, uliyepewa neema, Bwana yu pamoja nawe.


Kwa maana tunafahamu kwa sehemu; na tunafanya unabii kwa sehemu;


Basi wakuu hao wakatwaa katika vyakula vyao, wala wasitake shauri kinywani mwa BWANA.


Basi, hapo ishara hizi zitakapokutukia, fanya kama uonavyo vema; kwa kuwa Mungu yuko pamoja nawe.


Lakini BWANA akamwambia Samweli, Usimtazame uso wake, wala urefu wa kimo chake; kwa maana mimi nimemkataa. BWANA haangalii kama binadamu aangaliavyo; maana wanadamu huitazama sura ya nje, bali BWANA huutazama moyo.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo