Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Mambo ya Nyakati 17:16 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

16 Ndipo akaingia Daudi mfalme, akaketi mbele za BWANA; akasema Mimi ni nani, Ee BWANA Mungu, na nyumba yangu ni nini, hata umenileta hadi hapa?

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

16 Kisha mfalme Daudi akaingia ndani ya hema na kuketi mbele ya Mwenyezi-Mungu, halafu akaomba, “Mimi ni nani, ee Mwenyezi-Mungu, na nyumba yangu ni nini hata unitukuze hivi?

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

16 Kisha mfalme Daudi akaingia ndani ya hema na kuketi mbele ya Mwenyezi-Mungu, halafu akaomba, “Mimi ni nani, ee Mwenyezi-Mungu, na nyumba yangu ni nini hata unitukuze hivi?

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

16 Kisha mfalme Daudi akaingia ndani ya hema na kuketi mbele ya Mwenyezi-Mungu, halafu akaomba, “Mimi ni nani, ee Mwenyezi-Mungu, na nyumba yangu ni nini hata unitukuze hivi?

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

16 Ndipo Mfalme Daudi akaingia ndani, akaketi mbele za Mwenyezi Mungu, akasema: “Mimi ni nani, Ee Bwana Mwenyezi Mungu, na jamaa yangu ni nini, hata umenileta hadi hapa?

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

16 Ndipo Mfalme Daudi akaingia ndani, akaketi mbele za bwana, akasema: “Mimi ni nani, Ee bwana Mwenyezi Mungu, na jamaa yangu ni nini, hata umenileta mpaka hapa nilipo?

Tazama sura Nakili




1 Mambo ya Nyakati 17:16
15 Marejeleo ya Msalaba  

mimi sistahili hata kidogo hizo rehema zote na kweli yote uliyomfanyia mtumwa wako; maana nilivuka mto huo wa Yordani na fimbo yangu tu, na sasa nimekuwa makundi mawili.


Ndipo Daudi, mfalme, akaingia, akaketi mbele za BWANA, akasema, Mimi ni nani, Bwana MUNGU, na nyumba yangu ni nini, hata umenileta hadi hapa?


Basi Hezekia akaupokea waraka katika mikono ya wale wajumbe, akausoma; kisha Hezekia akapanda, akaingia katika nyumba ya BWANA, akaukunjua mbele za BWANA.


Kwa maneno hayo yote, na kwa maono hayo yote, ndivyo Nathani alivyonena na Daudi.


Tena jambo hili lilikuwa dogo machoni pako, Ee Mungu; hata umeleta habari ya nyumba yangu mimi, mtumishi wako, kwa miaka mingi inayokuja, nawe umeniangalia kama mtu mwenye cheo, Ee BWANA Mungu.


Lakini mimi ni nani, na watu wangu ni nani, hata tuweze kutoa kwa hiari hivi? Kwani vitu vyote vyatoka kwako na katika vitu vyako mwenyewe tumekutolea.


Sulemani akamwambia Mungu, Umemfanyia baba yangu Daudi fadhili kuu, nawe umenimilikisha mimi badala yake.


Ee BWANA, mtu ni kitu gani hata umjali? Na binadamu hata umwangalie?


Basi kwa kuwa nimeupata msaada utokao kwa Mungu nimesimama hata leo hivi nikiwashuhudia wadogo kwa wakubwa, wala sisemi neno ila yale ambayo manabii na Musa waliyasema, kwamba yatakuwa;


aliyetuokoa sisi katika mauti kuu namna ile; tena atatuokoa; ambaye tumemtumaini kuwa atazidi kutuokoa;


Mimi, niliye mdogo kuliko yeye aliye mdogo wa watakatifu wote, nilipewa neema hii ya kuwahubiria Mataifa utajiri wake Kristo usiopimika;


Akamwambia, Ee Bwana, nitawaokoa Israeli kwa jinsi gani? Tazama, jamaa zangu ndio walio maskini sana katika Manase, na mimi ndimi niliye mdogo katika nyumba ya baba yangu.


Ndipo Samweli akatwaa jiwe, na kulisimamisha kati ya Mispa na Sheni, akaliita jina lake Ebenezeri, akisema, Hata sasa BWANA ametusaidia.


Basi Sauli akajibu, akasema, Je! Mimi si Mbenyamini, mtu wa kabila iliyo ndogo kuliko kabila zote za Israeli? Na jamaa yangu nayo si ndogo kuliko jamaa zote za kabila la Benyamini? Kwa nini basi, kuniambia hivyo?


Tufuate:

Matangazo


Matangazo