Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Mambo ya Nyakati 17:11 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

11 Hata itakuwa, siku zako zitakapotimia, uende kulala pamoja na baba zako, nitainua mzawa wako nyuma yako, atakayekuwa wa wana wako; nami nitauimarisha ufalme wake.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

11 Siku zako zitakapotimia za kujiunga na babu zako, nitamfanya mmoja wa watoto wako, wewe mwenyewe awe mfalme; nami nitauimarisha ufalme wake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

11 Siku zako zitakapotimia za kujiunga na babu zako, nitamfanya mmoja wa watoto wako, wewe mwenyewe awe mfalme; nami nitauimarisha ufalme wake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

11 Siku zako zitakapotimia za kujiunga na babu zako, nitamfanya mmoja wa watoto wako, wewe mwenyewe awe mfalme; nami nitauimarisha ufalme wake.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

11 Siku zako zikiisha, nawe ukaenda kulala na baba zako, nitamwinua mzao wako kuwa mfalme baada yako, mmoja wa wana wako mwenyewe, nami nitauimarisha ufalme wake.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

11 Wakati wako utakapokuwa umekwisha, nawe ukawa umekwenda kukaa na baba zako, nitamwinua mzao wako aingie mahali pako kuwa mfalme, mmoja wa wana wako mwenyewe, nami nitaufanya imara ufalme wake.

Tazama sura Nakili




1 Mambo ya Nyakati 17:11
21 Marejeleo ya Msalaba  

Lakini wewe utakwenda kwa baba zako kwa amani, utazikwa katika uzee mwema.


Ama sivyo itakuwa, bwana wangu mfalme atakapolala pamoja na baba zake, mimi na mwanangu Sulemani tutahesabiwa kuwa wahalifu.


Basi Daudi akalala na babaze, akazikwa mjini mwa Daudi.


Lakini wewe hutanijengea nyumba hiyo; ila mwanao utakayemzaa wewe mwenyewe, yeye ndiye atakayeijenga nyumba kwa jina langu.


Basi BWANA amelitimiza neno lile alilolinena; nami nimesimama mahali pa Daudi baba yangu, na kuketi katika kiti cha enzi cha Israeli, kama BWANA alivyoahidi, nami nimeijenga nyumba kwa jina la BWANA, Mungu wa Israeli.


na tangu siku ile nilipowaamuru waamuzi wawatawale watu wangu Israeli, nami nitawashinda adui zako wote. Pamoja na hayo nakuambia, ya kwamba BWANA atakujengea nyumba.


Yeye ndiye atakayenijengea nyumba, nami nitakiimarisha kiti cha enzi cha ufalme wake milele.


tena katika wana wangu wote (kwani BWANA amenipa wana wengi), amemchagua Sulemani mwanangu ili aketi juu ya kiti cha enzi cha ufalme wa BWANA, juu ya Israeli.


Kwani sisi tu wageni na wapitaji mbele zako, kama walivyokuwa baba zetu wote; siku zetu duniani ni kama kivuli, na hakuna tumaini la kuishi.


Akafa akiwa mzee sana, mwenye maisha marefu, mali na heshima; naye Sulemani mwanawe akatawala badala yake.


lakini si wewe utakayeijenga nyumba hiyo; ila mwanao atakayetoka katika uzao wako, yeye ndiye atakayejenga nyumba kwa jina langu.


BWANA amemwapia Daudi neno la kweli, Hatarudi nyuma akalivunja, Mmoja wa wazawa wako mwenyewe Nitawaweka katika kiti chako cha enzi.


Ee BWANA, mbingu zitayasifu maajabu yako, Uaminifu wako katika kusanyiko la watakatifu.


Maana BWANA asema hivi, Daudi hatakosa kuwa na mtu wa kuketi katika kiti cha enzi cha nyumba ya Israeli;


Kwa maana Daudi, akiisha kulitumikia shauri la Mungu katika kizazi chake, alilala, akawekwa pamoja na baba zake, akaona uharibifu.


Wanaume, ndugu zangu, mniwie radhi, niseme kwa ujasiri mbele yenu habari za baba yetu mkuu, Daudi, ya kuwa alifariki akazikwa, na kaburi lake liko kwetu hata leo.


BWANA akamwambia Musa, Angalia, wewe utalala na baba zako; na watu hawa wataondoka, wataifuata kwa ukahaba miungu ya kigeni ya nchi waiendeayo kuwa kati yao, nao wataniacha mimi na kulivunja agano langu, nililofanya nao.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo