Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Mambo ya Nyakati 17:1 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

1 Ikawa, Daudi alipokuwa akikaa nyumbani mwake, Daudi akamwambia nabii Nathani, Angalia, mimi ninakaa katika nyumba ya mwerezi, bali sanduku la Agano la BWANA linakaa chini ya mapazia.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

1 Wakati mfalme Daudi alipokuwa akikaa katika ikulu, siku moja alimwita nabii Nathani, na kumwambia, “Hebu tazama, mimi ninakaa kwenye nyumba nzuri iliyojengwa kwa mwerezi, lakini sanduku la agano la Mwenyezi-Mungu linakaa hemani.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

1 Wakati mfalme Daudi alipokuwa akikaa katika ikulu, siku moja alimwita nabii Nathani, na kumwambia, “Hebu tazama, mimi ninakaa kwenye nyumba nzuri iliyojengwa kwa mwerezi, lakini sanduku la agano la Mwenyezi-Mungu linakaa hemani.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

1 Wakati mfalme Daudi alipokuwa akikaa katika ikulu, siku moja alimwita nabii Nathani, na kumwambia, “Hebu tazama, mimi ninakaa kwenye nyumba nzuri iliyojengwa kwa mwerezi, lakini sanduku la agano la Mwenyezi-Mungu linakaa hemani.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

1 Baada ya Daudi kuingia rasmi katika jumba lake la kifalme, akamwambia nabii Nathani, “Hebu tazama, mimi ninakaa kwenye nyumba nzuri iliyojengwa kwa mwerezi, wakati Sanduku la Agano la Mwenyezi Mungu liko ndani ya hema.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

1 Baada ya Daudi kuingia rasmi katika jumba lake la kifalme, akamwambia nabii Nathani, “Hebu tazama, mimi ninakaa kwenye nyumba nzuri iliyojengwa kwa mierezi, wakati Sanduku la Agano la bwana liko ndani ya hema.”

Tazama sura Nakili




1 Mambo ya Nyakati 17:1
28 Marejeleo ya Msalaba  

Ndipo BWANA akamtuma Nathani aende kwa Daudi. Naye akamwendea, akamwambia, Palikuwa na watu wawili katika mji mmoja; mmoja wao alikuwa tajiri, wa pili maskini.


akapeleka kwa mkono wa Nathani, nabii, naye akamwita jina lake Yedidia, kwa ajili ya BWANA.


Wakaliingiza sanduku la BWANA, na kuliweka mahali pake, katikati ya hema aliyoipiga Daudi kwa ajili yake, naye Daudi akatoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani mbele za BWANA.


Wakamwambia mfalme wakasema, Tazama, Nathani, nabii. Naye alipoingia ndani mbele ya mfalme, akamsujudia kifudifudi.


Tena mfalme alipeleka pamoja naye Sadoki, kuhani, na Nathani, nabii, na Benaya, mwana wa Yehoyada, na Wakerethi, na Wapelethi, wakampandisha juu ya nyumbu wa mfalme.


Ila Sadoki, kuhani, na Benaya, mwana wa Yehoyada, na Nathani, nabii, na Shimei, na Rei, na mashujaa wa Daudi, hao hawakuwa pamoja na Adonia.


Basi ilikuwa moyoni mwake Daudi, baba yangu, kujenga nyumba kwa jina la BWANA, Mungu wa Israeli.


Naye Hiramu, mfalme wa Tiro, akatuma wajumbe kwa Daudi, akampelekea na mierezi, na waashi, na maseremala, ili wamjengee nyumba.


Basi Daudi akajijengea nyumba katika mji wa Daudi; akatayarisha mahali kwa ajili ya sanduku la Mungu, akalipigia hema.


Wakaliingiza sanduku la Mungu, na kuliweka katikati ya hema aliyoipiga Daudi kwa ajili yake; wakatoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani mbele za Mungu.


Naye Nathani akamwambia Daudi, Haya, fanya yote yaliyomo moyoni mwako; kwa maana Mungu yu pamoja nawe.


kwa maana sikukaa ndani ya nyumba tangu siku ile nilipowaleta Israeli huku hata leo; lakini hema kwa hema nimehamia, na maskani kwa maskani.


Ndipo akamwita Sulemani mwanawe, akamwagiza amjengee BWANA, Mungu wa Israeli, nyumba.


Daudi akamwambia Sulemani mwanawe, Kwangu mimi nia yangu ilikuwa kujenga nyumba kwa ajili ya jina la BWANA, Mungu wangu.


Ndipo Daudi mfalme akasimama kwa miguu yake, akasema, Nisikilizeni, ndugu zangu, na watu wangu; Mimi nilikuwa na nia ya kuijenga nyumba ya kuliweka sanduku la Agano la BWANA, na kiti cha kuwekea miguu cha Mungu wetu; hata nilikuwa nimejitayarisha kujenga.


Basi habari za mfalme Daudi, mwanzo hadi mwisho, angalia, zimeandikwa katika kumbukumbu za Samweli, mwonaji, na katika kumbukumbu za Nathani, nabii, na katika kumbukumbu za Gadi, mwonaji;


Lakini sanduku la Mungu, Daudi alikuwa amelipandisha kutoka Kiriath-yearimu mpaka mahali Daudi alipolitengenezea; maana amelitandia hema katika Yerusalemu.


Hadi nitakapompatia BWANA mahali, Na Mwenye nguvu wa Yakobo maskani”.


Kisha fanya hiyo maskani iwe na mapazia kumi; ifanye ya nguo ya kitani nzuri ya kusokota, pamoja na nyuzi za rangi ya buluu, zambarau na nyekundu, pamoja na makerubi; kazi ya fundi stadi.


Je! Utatawala kwa sababu unashindana na watu kwa mierezi? Baba yako, je! Hakula na kunywa, na kufanya hukumu na haki? Hapo ndipo alipofanikiwa.


Mimi, Nebukadneza, nilikuwa nikistarehe nyumbani kwangu, nikineemeka katika nyumba yangu ya enzi.


Je! Huu ndio wakati wa ninyi kukaa katika nyumba zenye mapambo ya mbao, iwapo nyumba hii inakaa hali ya kuharibika?


Mlitazamia vingi, kumbe vikatokea vichache; tena mlipovileta nyumbani nikavipeperusha mbali. Ni kwa sababu gani? Asema BWANA wa majeshi. Ni kwa sababu yumba yangu imebaki kuwa gofu la nyumba, wakati ambapo kila mmoja wenu anakimbilia nyumbani kwake.


aliyepata fadhili mbele za Mungu, naye aliomba ampatie Mungu wa Yakobo maskani.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo