Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Mambo ya Nyakati 16:31 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

31 Mbingu na zifurahi, nchi na ishangilie; Na waseme katika mataifa, BWANA ametamalaki;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

31 Furahini enyi mbingu na dunia! Yaambieni mataifa, “Mwenyezi-Mungu anatawala!”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

31 Furahini enyi mbingu na dunia! Yaambieni mataifa, “Mwenyezi-Mungu anatawala!”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

31 Furahini enyi mbingu na dunia! Yaambieni mataifa, “Mwenyezi-Mungu anatawala!”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

31 Mbingu na zishangilie, nchi na ifurahi; semeni katika mataifa, “Mwenyezi Mungu anatawala!”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

31 Mbingu na zishangilie, nchi na ifurahi; semeni katikati ya mataifa, “bwana anatawala!”

Tazama sura Nakili




1 Mambo ya Nyakati 16:31
19 Marejeleo ya Msalaba  

Tetemekeni mbele zake, nchi yote. Naam, ulimwengu umethibitika usitikisike;


Ee Mungu wangu, Mfalme, nitakutukuza, Nitalihimidi jina lako milele na milele.


Mbingu zauhubiri utukufu wa Mungu, Na anga laitangaza kazi ya mikono yake.


Mungu ayatawala mataifa, Mungu ameketi katika kiti chake kitakatifu.


Ee BWANA, mbingu zitayasifu maajabu yako, Uaminifu wako katika kusanyiko la watakatifu.


Semeni katika mataifa, BWANA ametamalaki; Naam, ulimwengu umethibitika usitikisike, Atawahukumu watu kwa adili.


BWANA ametamalaki, nchi na ishangilie, Visiwa vingi na vifurahi.


Mshangilieni BWANA, nchi yote, Inueni sauti, imbeni kwa furaha, imbeni sifa.


BWANA ametamalaki, mataifa wanatetemeka; Ameketi juu ya makerubi, nchi inatikisika.


Kwa maana BWANA ndiye mwamuzi wetu; BWANA ndiye mfanya sheria wetu; BWANA ndiye mfalme wetu; ndiye atakayetuokoa.


Imbeni, enyi mbingu, maana BWANA ametenda hayo; Pigeni kelele, enyi mabonde ya nchi; Pazeni nyimbo, enyi milima; Nawe, msitu, na kila mti ndani yake. Maana BWANA amemkomboa Yakobo, Naye atajitukuza katika Israeli.


Imbeni, enyi mbingu; ufurahi, Ee nchi; Pazeni sauti ya kuimba, enyi milima; Kwa kuwa BWANA amewafariji watu wake, Naye atawahurumia watu wake walioteswa.


Na usitutie majaribuni, lakini utuokoe na yule mwovu. [Kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu, na utukufu, hata milele. Amina.]


Nawaambia, Vivyo hivyo kuna furaha mbele ya malaika wa Mungu kwa ajili ya mwenye dhambi mmoja atubuye.


Malaika akawaambia, Msiogope; kwa kuwa mimi ninawaletea habari njema ya furaha kuu itakayokuwa kwa watu wote;


Nikasikia sauti kama sauti ya makutano mengi, na kama sauti ya maji mengi, na kama sauti ya radi yenye nguvu, ikisema, Haleluya; kwa kuwa Bwana Mungu wetu, Mwenyezi, amemiliki.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo