Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Mambo ya Nyakati 16:29 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

29 Mpeni BWANA utukufu wa jina lake; Leteni sadaka, na mje mbele zake; Mwabuduni BWANA kwa uzuri wa utakatifu;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

29 Mpeni Mwenyezi-Mungu heshima ya utukufu wa jina lake; leteni tambiko na kuingia nyumbani mwake. Mwabuduni Mwenyezi-Mungu patakatifuni pake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

29 Mpeni Mwenyezi-Mungu heshima ya utukufu wa jina lake; leteni tambiko na kuingia nyumbani mwake. Mwabuduni Mwenyezi-Mungu patakatifuni pake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

29 Mpeni Mwenyezi-Mungu heshima ya utukufu wa jina lake; leteni tambiko na kuingia nyumbani mwake. Mwabuduni Mwenyezi-Mungu patakatifuni pake.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

29 mpeni Mwenyezi Mungu utukufu unaostahili jina lake. Leteni sadaka na mje katika nyua zake. Mwabuduni Mwenyezi Mungu katika uzuri wa utakatifu wake.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

29 mpeni bwana utukufu unaostahili jina lake. Leteni sadaka na mje katika nyua zake; mwabuduni bwana katika uzuri wa utakatifu wake.

Tazama sura Nakili




1 Mambo ya Nyakati 16:29
28 Marejeleo ya Msalaba  

Mpeni BWANA, enyi jamaa za watu, Mpeni BWANA utukufu na nguvu.


Tetemekeni mbele zake, nchi yote. Naam, ulimwengu umethibitika usitikisike;


Naye alipokwisha kufanya shauri na watu, akawaweka wale watakaomwimbia BWANA, na kumsifu katika uzuri wa utakatifu, wakitoka mbele ya jeshi, na kusema, Mshukuruni BWANA; kwa maana fadhili zake ni za milele.


Ingieni malangoni mwake kwa shukrani; Nyuani mwake kwa kusifu; Mshukuruni, lihimidini jina lake;


Watu wako watajitoa kwa hiari, Siku ya uwezo wako; Kwa uzuri wa utakatifu, Tokea tumbo la asubuhi, Unao umande wa ujana wako.


Mpeni BWANA, enyi wana wa Mungu, Mpeni BWANA utukufu na nguvu;


Mpeni BWANA utukufu wa jina lake; Mwabuduni BWANA kwa uzuri wa utakatifu.


Tokea Sayuni, ukamilifu wa uzuri, Mungu ameangaza kote.


Wafalme wa Tarshishi na visiwa na walete kodi; Wafalme wa Sheba na Seba na watoe vipawa.


Na aishi maisha marefu! Na wampe dhahabu ya Sheba; Na wamwombee daima; Na kumbariki mchana kutwa.


Tuje mbele zake kwa shukrani, Tumfanyie shangwe kwa zaburi.


Heshima na adhama ziko mbele zake, Nguvu na uzuri zimo katika patakatifu pake.


Mpeni BWANA, enyi jamaa za watu, Mpeni BWANA utukufu na nguvu.


Mwabuduni BWANA kwa uzuri wa utakatifu, Tetemekeni mbele zake, nchi yote.


Amka, amka, jivike nguvu zako, Ee Sayuni; Jivike mavazi yako mazuri, Ee Yerusalemu, mji mtakatifu; Kwa maana tokea sasa hataingia ndani yako Asiyetahiriwa, wala aliye najisi.


Wakaitana, kila mmoja na mwenzake, wakisema, Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, ni BWANA wa majeshi; dunia yote imejaa utukufu wake.


Nawe, mwanadamu, je! Haitakuwa hivi katika siku hiyo nitakapowaondolea nguvu zao, na furaha ya utukufu wao, na kilichotamaniwa na macho yao, ambacho walikiinulia mioyo yao, watoto wao wa kiume na watoto wao wa kike,


Na uzuri wa pambo lake, yeye aliuweka katika enzi, lakini wao walifanya sanamu za machukizo yao, na vitu vyao vichukizavyo, ndani yake; ndiyo maana nimeifanya kuwa kama kitu cha unajisi kwao.


wakisema, Amina; Baraka na utukufu na hekima na shukrani na heshima na uweza na nguvu zina Mungu wetu hata milele na milele. Amina.


Kwa hiyo mtafanya sanamu za majipu yenu, na sanamu za panya wenu wanaoiharibu nchi; nanyi mtamtukuza huyo Mungu wa Israeli; huenda ataupunguza uzito wa mkono wake juu yenu, na juu ya miungu yenu, na juu ya nchi yenu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo