Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Mambo ya Nyakati 16:25 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

25 Kwa kuwa BWANA ni mkuu mwenye kusifiwa sana; Na wa kuhofiwa kuliko miungu yote.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

25 Maana Mwenyezi-Mungu ni mkuu, anasifika sana anastahili kuheshimiwa kuliko miungu yote.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

25 Maana Mwenyezi-Mungu ni mkuu, anasifika sana anastahili kuheshimiwa kuliko miungu yote.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

25 Maana Mwenyezi-Mungu ni mkuu, anasifika sana anastahili kuheshimiwa kuliko miungu yote.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

25 Kwa kuwa Mwenyezi Mungu ni mkuu, mwenye kustahili kusifiwa kuliko wote; yeye ni wa kuogopwa kuliko miungu yote.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

25 Kwa kuwa bwana ni mkuu, mwenye kustahili kusifiwa kuliko wote; yeye ni wa kuogopwa kuliko miungu yote.

Tazama sura Nakili




1 Mambo ya Nyakati 16:25
15 Marejeleo ya Msalaba  

Watangazieni mataifa habari za utukufu wake, Na watu wote habari za maajabu yake.


Nayo nyumba nitakayoijenga ni kubwa; kwa sababu Mungu wetu ndiye mkuu juu ya miungu yote.


BWANA ndiye mkuu mwenye kusifiwa sana, Wala ukuu wake hauchunguziki.


Bwana ndiye aliye mkuu, Na mwenye kusifiwa sana. Katika mji wa Mungu wetu, Katika mlima wake mtakatifu.


Wewe ndiwe utishaye, naam, Wewe; Naye ni nani awezaye kusimama ukasirikapo?


Toka mbinguni ulitangaza hukumu; Nchi iliogopa, ikakaa kimya.


Mungu huogopwa sana barazani pa watakatifu, Ni wa kuhofiwa kuliko wote wanaomzunguka.


Ee BWANA, katika miungu ni nani aliye kama wewe? Ni nani aliye kama wewe, mtukufu katika utakatifu, Mwenye kuogopwa katika sifa zako, mfanya maajabu?


Je! Hamniogopi mimi? Asema BWANA; hamtatetemeka mbele za uso wangu; mimi niliyeweka mchanga kuwa mpaka wa bahari, kwa amri ya daima, isiweze kuupita? Mawimbi yake yajapoumuka-umuka, hayawezi kushinda nguvu; yajapovuma sana, hayawezi kuupita.


Kwa maana tokea maawio ya jua hata machweo yake jina langu ni kuu katika mataifa; na katika kila mahali unatolewa uvumba na dhabihu safi kwa jina langu; maana jina langu ni kuu katika mataifa, asema BWANA wa majeshi.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo