Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Mambo ya Nyakati 16:16 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

16 Agano alilofanya na Abrahamu, Na kiapo chake kwa Isaka;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

16 Hushika agano alilofanya na Abrahamu, na ahadi aliyomwapia Isaka.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

16 Hushika agano alilofanya na Abrahamu, na ahadi aliyomwapia Isaka.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

16 Hushika agano alilofanya na Abrahamu, na ahadi aliyomwapia Isaka.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

16 agano alilolifanya na Ibrahimu, kiapo alichomwapia Isaka.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

16 agano alilolifanya na Ibrahimu, kiapo alichomwapia Isaka.

Tazama sura Nakili




1 Mambo ya Nyakati 16:16
16 Marejeleo ya Msalaba  

BWANA akamtokea Abramu, akasema, Uzao wako nitawapa nchi hii. Naye akamjengea BWANA madhabahu huko alikomtokea.


Siku ile BWANA akafanya agano na Abramu, akasema, Uzao wako nimewapa nchi hii, kutoka mto wa Misri mpaka huo mto mkubwa, mto Frati,


Nami nitafanya agano langu nawe, nami nitakuzidishia sana.


Kaa ugenini katika nchi hiyo, nami nitakuwa pamoja nawe, na kukubariki, maana nitakupa wewe na uzao wako nchi hizi zote. Nami nitakifanya imara kiapo nilichomwapia Abrahamu baba yako.


Mungu akamwambia, Mimi ni Mungu Mwenyezi, uzidi ukaongezeke. Taifa na kundi la mataifa watatoka kwako, na wafalme watatoka katika uzao wako.


Kisha mfalme Daudi akaambiwa ya kwamba, BWANA ameibariki nyumba ya Obed-edomu, na vitu vyote alivyo navyo kwa ajili ya sanduku la Mungu. Daudi akaenda, akalileta sanduku la Mungu, toka nyumba ya Obed-edomu mpaka mji wa Daudi, kwa shangwe.


Likumbukeni agano lake milele, Neno lile aliloviamuru vizazi elfu.


nawe ukauona moyo wake kuwa mwaminifu mbele zako, ukafanya agano naye, kumpa nchi ya Mkanaani, na Mhiti, na Mwamori, na Mperizi, na Myebusi, na Mgirgashi, naam, kuwapa wazao wake; nawe umetimiza ahadi yako kwani u mwenye haki.


Tena Mungu akamwambia Musa, Waambie wana wa Israeli maneno haya, BWANA, Mungu wa baba zenu, Mungu wa Abrahamu, Mungu wa Isaka, Mungu wa Yakobo, amenituma kwenu; hili ndilo jina langu hata milele, nalo ni kumbukumbu langu hata vizazi vyote.


Ninyi mmekuwa watoto wa manabii na wa maagano yale, ambayo Mungu aliagana na baba zenu, akimwambia Abrahamu, Katika uzao wako kabila zote za ulimwengu zitabarikiwa.


bali kwa sababu BWANA anawapenda, na kwa sababu alitaka kukitimiza kiapo chake alichowaapia baba zenu, ndiyo sababu BWANA akawatoa kwa mkono wa nguvu, akawakomboa katika nyumba ya utumwa, katika mkono wa Farao, mfalme wa Misri.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo