Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Mambo ya Nyakati 15:25 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

25 Basi Daudi, na wazee wa Israeli, na makamanda wa maelfu, wakaenda, ili kulipandisha sanduku la Agano la BWANA kutoka nyumbani mwa Obed-edomu kwa furaha kuu;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

25 Basi, Daudi, wazee wa Waisraeli na makamanda wa maelfu, wakaenda kulichukua sanduku la agano la Mwenyezi-Mungu kutoka nyumbani kwa Obed-edomu kwa shangwe.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

25 Basi, Daudi, wazee wa Waisraeli na makamanda wa maelfu, wakaenda kulichukua sanduku la agano la Mwenyezi-Mungu kutoka nyumbani kwa Obed-edomu kwa shangwe.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

25 Basi, Daudi, wazee wa Waisraeli na makamanda wa maelfu, wakaenda kulichukua sanduku la agano la Mwenyezi-Mungu kutoka nyumbani kwa Obed-edomu kwa shangwe.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

25 Basi Daudi pamoja na wazee wa Israeli na majemadari wa vikosi vya elfu wakaenda ili kulipandisha Sanduku la Agano la Mwenyezi Mungu kutoka nyumba ya Obed-Edomu kwa shangwe.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

25 Basi Daudi pamoja na wazee wa Israeli na majemadari wa vikosi vya elfu wakaenda ili kulipandisha Sanduku la Agano la bwana kutoka nyumba ya Obed-Edomu kwa shangwe.

Tazama sura Nakili




1 Mambo ya Nyakati 15:25
21 Marejeleo ya Msalaba  

Ndipo Sulemani alipowakusanya wazee wa Israeli, na wakuu wote wa makabila na wakuu wa koo za wana wa Israeli, wamwendee mfalme Sulemani huko Yerusalemu, ili walipandishe sanduku la Agano la BWANA kutoka mji wa Daudi, yaani, Sayuni.


Lakini sanduku la Mungu, Daudi alikuwa amelipandisha kutoka Kiriath-yearimu mpaka mahali Daudi alipolitengenezea; maana amelitandia hema katika Yerusalemu.


Ndipo Sulemani alipowakusanya wazee wa Israeli, na wakuu wote wa kabila, wakuu wa mbari za mababa wa wana wa Israeli, huko Yerusalemu, ili walipandishe sanduku la Agano la BWANA kutoka mji wa Daudi, yaani, Sayuni.


Na wana wa Israeli, na makuhani na Walawi, na watu wengine katika hao waliohamishwa, wakaiweka wakfu nyumba ya Mungu kwa furaha.


Bali wewe, Bethlehemu Efrata, uliye mdogo kuwa miongoni mwa elfu za Yuda; kutoka kwako wewe atanitokea mmoja atakayekuwa mtawala katika Israeli; ambaye asili yake imekuwa tangu zamani za kale, tangu milele.


Musa akawakasirikia majemadari wa jeshi, na hao makamanda wa maelfu, na makamanda wa mamia, hao waliorudi kutoka kupigana vita.


Basi nikatwaa vichwa vya makabila yenu wenye akili, waliojulikana, nikawafanya wawe vichwa juu yenu, makamanda wa maelfu, na makamanda wa mamia, na makamanda wa hamsini hamsini, na makamanda wa kumi kumi, na wenye amri, kwa kadiri ya makabila yenu.


lakini hivyo mtakula mbele za BWANA, Mungu wako, mahali atakapochagua BWANA, Mungu wako, wewe, na mwanao wa kiume na wa kike, na mtumwa wako mume na mke, na Mlawi aliye ndani ya malango yako; nawe furahi mbele za BWANA, Mungu wako, katika yote utakayotia mkono wako.


na huko mtakula mbele za BWANA, Mungu wenu, nanyi furahini katika yote mtakayotia mikono yenu, ninyi na wa nyumbani mwenu, aliyokubarikia BWANA, Mungu wako.


nawe utafurahi mbele ya BWANA, Mungu wako, wewe na mwana wako na binti yako, na mtumwa wako na mjakazi wako, na Mlawi aliye ndani ya malango yako, na mgeni, na yatima, na mjane aliyefiliwa na mumewe, walio katikati yako, katika mahali atakapochagua BWANA, Mungu wako, apakalishe jina lake.


Siku saba mfanyie sikukuu BWANA, Mungu wako, mahali atakapochagua BWANA; kwa kuwa BWANA, Mungu wako, atakubariki katika mavuno yako yote, na katika kazi zote za mikono yako, nawe uwe katika kufurahi kabisa.


Maana sisi tu tohara, tumwabuduo Mungu kwa Roho, na kuona fahari juu ya Kristo Yesu, wala hatuutumainii mwili.


Furahini katika Bwana sikuzote; tena nasema, Furahini.


lakini leo mmemkataa Mungu wenu, naye ndiye awaponyaye katika misiba yenu yote na shida zenu; nanyi mmemwambia, Sivyo, lakini weka mfalme juu yetu. Basi, sasa, njoni mbele za BWANA, kwa makabila yenu na kwa maelfu yenu.


Naye Sauli akawaambia watumishi wake waliomzunguka, Sikieni sasa, enyi Wabenyamini; je! Huyu mwana wa Yese atawapa ninyi kila mmoja mashamba, na mashamba ya mizabibu, atawafanya kuwa wakuu wa watu maelfu, na wakuu wa watu mamia;


Naye atawaweka kwake kuwa wakuu juu ya maelfu, na makamanda juu ya hamsini hamsini; na wengine atawaweka walime shamba lake, na kuvuna mavuno yake, na kufanyiza zana zake za vita, na vyombo vya magari yake.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo