Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Mambo ya Nyakati 15:17 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

17 Basi Walawi wakamwagiza Hemani mwana wa Yoeli; na wa nduguze, Asafu mwana wa Berekia; na wa wana wa Merari ndugu zao, Ethani mwana wa Kishi;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

17 Hivyo wakachagua watu wafuatao katika koo za waimbaji: Hemani mwana wa Yoeli, Asafu nduguye aliyekuwa mwana wa Berekia na wana wa Merari, ndugu zao, na Ethani mwana wa Kushaya.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

17 Hivyo wakachagua watu wafuatao katika koo za waimbaji: Hemani mwana wa Yoeli, Asafu nduguye aliyekuwa mwana wa Berekia na wana wa Merari, ndugu zao, na Ethani mwana wa Kushaya.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

17 Hivyo wakachagua watu wafuatao katika koo za waimbaji: Hemani mwana wa Yoeli, Asafu nduguye aliyekuwa mwana wa Berekia na wana wa Merari, ndugu zao, na Ethani mwana wa Kushaya.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

17 Basi Walawi wakawateua Hemani mwana wa Yoeli; kutoka miongoni mwa ndugu zake, Asafu mwana wa Berekia; kutoka miongoni mwa ndugu zao Wamerari, Ethani mwana wa Kushaiya;

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

17 Basi Walawi wakawaweka Hemani mwana wa Yoeli; kutoka miongoni mwa ndugu zake, Asafu mwana wa Berekia; kutoka miongoni mwa ndugu zao Wamerari, Ethani mwana wa Kushaiya;

Tazama sura Nakili




1 Mambo ya Nyakati 15:17
15 Marejeleo ya Msalaba  

na pamoja nao ndugu zao kwa cheo cha pili, Zekaria, na Yaasieli, na Shemiramothi, na Yehieli, na Uni, na Eliabu; na Benaya, na Maaseya, na Matithia, na Elifelehu, na Mikneya, na Obed-edomu, na Yeieli, mabawabu.


Hivyo hao waimbaji, Hemani, Asafu, na Ethani, wakaagizwa kupiga matoazi yao ya shaba kwa sauti kuu;


na pamoja nao Hemani na Yeduthuni, na wale wengine waliochaguliwa, waliotajwa majina yao, ili kumshukuru BWANA, kwa kuwa fadhili zake ni za milele;


na pamoja nao Hemani na Yeduthuni wenye baragumu na matoazi, kwa hao watakaovumisha sauti, na vinanda kwa ajili ya hizo nyimbo za Mungu; na hao wana wa Yeduthuni wawepo mlangoni.


Na wana wa Kohathi walikuwa Amramu, na Ishari, na Hebroni, na Uzieli.


na mwanawe huyo ni Tahathi, na mwanawe huyo ni Urieli, na mwanawe huyo ni Uzia, na mwanawe huyo ni Shauli.


Wana wa Merari; Mali, na mwanawe huyo ni Libni, na mwanawe huyo ni Shimei, na mwanawe huyo ni Uza;


Na hawa ndio waliohudumu pamoja na wana wao. Katika wana wa Wakohathi; Hemani mwimbaji, mwana wa Yoeli, mwana wa Samweli;


Na nduguye Asafu, aliyesimama upande wake wa kulia, huyo Asafu alikuwa mwana wa Berekia, mwana wa Shimea;


Na upande wa kushoto ndugu zao, wana wa Merari; Ethani, mwana wa Kishi, mwana wa Abdi, mwana wa Maluki;


Mungu, Mungu BWANA, amenena, ameiita nchi, Toka maawio ya jua hadi machweo yake.


Hakika Mungu ni mwema kwa Israeli, Kwa hao walio safi mioyo yao.


Ee Mungu, usistarehe, Ee Mungu, usinyamae, wala usitulie.


Na jina la mwanawe mzaliwa wa kwanza lilikuwa Yoeli; na jina la wa pili Abiya; walikuwa waamuzi katika Beer-sheba.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo