Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Mambo ya Nyakati 13:1 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

1 Kisha Daudi akafanya shauri na makamanda wa maelfu, na makamanda wa mamia, naam, na kila kiongozi.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

1 Daudi alishauriana na makamanda wa vikosi vya maelfu na vikosi vya mamia, pamoja na viongozi wote.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

1 Daudi alishauriana na makamanda wa vikosi vya maelfu na vikosi vya mamia, pamoja na viongozi wote.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

1 Daudi alishauriana na makamanda wa vikosi vya maelfu na vikosi vya mamia, pamoja na viongozi wote.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

1 Daudi alishauriana na kila kiongozi wake, majemadari wa maelfu na majemadari wa mamia.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

1 Daudi alishauriana na kila afisa wake, majemadari wa maelfu na majemadari wa mamia.

Tazama sura Nakili




1 Mambo ya Nyakati 13:1
12 Marejeleo ya Msalaba  

Basi Daudi akakusanya tena wateule wote wa Israeli, watu elfu thelathini.


Kisha, mfalme akatuma wajumbe, nao wakamkusanyia wazee wote wa Yuda na wa Yerusalemu.


Hao Wagadi walikuwa makamanda wa jeshi, yeye aliyekuwa mdogo amelingana na mia moja, na yeye aliyekuwa mkuu, na elfu moja.


Naye alipokuwa akienda Siklagi, Manase hawa wakamwangukia, Adna, na Yozabadi, na Yediaeli, na Mikaeli, na Yozabadi, na Elihu, na Silethai, makamanda wa maelfu waliokuwa wa Manase.


Na wa wana wa Isakari, watu wenye akili za kujua nyakati, kuyajua yawapasayo Israeli wayatende; vichwa vyao walikuwa watu mia mbili na ndugu zao wote walikuwa chini ya amri yao.


Zaidi ya hayo, wale waliokuwa karibu nao, hata mpaka kwa Isakari, na Zabuloni, na Naftali, wakaleta chakula juu ya punda, na ngamia, na nyumbu, na ng'ombe, vyakula vya unga, mikate ya tini, na vichala vya zabibu kavu, na divai, na mafuta, na ng'ombe, na kondoo tele; kwa kuwa kulikuwa na furaha katika Israeli.


Daudi akawaambia jamii yote ya Israeli, Likiwa jema kwenu, tena likiwa limetoka kwa BWANA, Mungu wetu, na tutume watu huku na huku mahali pote kwa ndugu zetu waliosalia katika nchi yote ya Israeli, ambao pamoja nao makuhani na Walawi wamo ndani ya miji yao yenye viunga, ili wakusanyike kwetu;


Sulemani akawaita Israeli wote, na makamanda wa maelfu, na wa mamia, na waamuzi, na kila kiongozi wa Israeli, na wakuu wa familia.


Ndipo Hezekia mfalme akaamka mapema, akakusanya wakuu wa mji, akapanda nyumbani kwa BWANA.


Pasipo ushauri mipango vuhunjika; Bali kwa wingi wa washauri huthibitika.


Mara yule aliyepokea talanta tano akaenda, akafanya biashara nazo, akachuma faida talanta nyingine tano.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo