Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




1 Mambo ya Nyakati 12:8 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

8 Na wa Wagadi wakajitenga kumfuata Daudi ngomeni huko nyikani, wanaume mashujaa, watu waliozoea vita, walioweza kutumia ngao na mkuki; ambao nyuso zao zilikuwa kama nyuso za simba, nao walikuwa wepesi kama kulungu juu ya milima;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

8 Tena, watu kutoka kabila la Gadi walijiunga na Daudi akiwa ngomeni kule nyikani. Hawa walikuwa askari wenye nguvu na uzoefu, hodari wa kutumia ngao na mkuki; wenye nyuso za kutisha kama simba na wepesi kama swala milimani.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

8 Tena, watu kutoka kabila la Gadi walijiunga na Daudi akiwa ngomeni kule nyikani. Hawa walikuwa askari wenye nguvu na uzoefu, hodari wa kutumia ngao na mkuki; wenye nyuso za kutisha kama simba na wepesi kama swala milimani.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

8 Tena, watu kutoka kabila la Gadi walijiunga na Daudi akiwa ngomeni kule nyikani. Hawa walikuwa askari wenye nguvu na uzoefu, hodari wa kutumia ngao na mkuki; wenye nyuso za kutisha kama simba na wepesi kama swala milimani.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

8 Baadhi ya Wagadi wakajitenga na kujiunga na Daudi katika ngome yake huko jangwani. Walikuwa mashujaa hodari, wakiwa wamejiandaa kwa vita, na wenye uwezo wa kutumia ngao na mkuki. Nyuso zao zilikuwa nyuso za simba na walikuwa na wepesi kama paa milimani.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

8 Baadhi ya Wagadi wakajitenga na kujiunga na Daudi katika ngome yake huko jangwani. Walikuwa mashujaa hodari, waliokuwa tayari kwa vita na wenye uwezo wa kutumia ngao na mkuki. Nyuso zao zilikuwa nyuso za simba na walikuwa na wepesi kama paa milimani.

Tazama sura Nakili




1 Mambo ya Nyakati 12:8
17 Marejeleo ya Msalaba  

Sauli na Yonathani walipendwa na kupendeza Maishani wala mautini hawakutengwa; Walikuwa wepesi kuliko tai, Walikuwa hodari kuliko simba.


Basi hata yeye aliye shujaa, mwenye moyo kama moyo wa simba, atayeyuka kabisa; maana Israeli wote wanajua ya kuwa baba yako ni shujaa, na ya kuwa watu wale walio pamoja naye ni mashujaa.


Na wana watatu wa Seruya walikuwako huko, Yoabu, na Abishai, na Asaheli; na Asaheli alikuwa mwepesi wa miguu kama kulungu.


Tena Benaya, mwana wa Yehoyada, mtu hodari wa Kabseeli aliyekuwa amefanya mambo makuu; aliwaua simba wawili wakali wa Moabu, pia aliingia katika shimo na kumwua simba wakati wa theluji;


Na Daudi wakati ule alikuwako ngomeni, na walinzi wa Wafilisti wakati ule walikuwa huko Bethlehemu.


Tena, Benaya, mwana wa Yehoyada, mtu hodari, wa Kabseeli, aliyekuwa amefanya mambo makuu, ndiye aliyewaua simba wakali wawili wa Moabu; pia akashuka, akamwua simba katikati ya shimo wakati wa theluji.


Tena wakafika ngomeni kwa Daudi baadhi ya wana wa Benyamini na Yuda.


na Yoela, na Zebadia, wana wa Yerohamu, wa Gedori.


Ezeri mkubwa wao, Obadia wa pili, Eliabu wa tatu;


Tena Amazia akawakusanya Yuda, akawaweka kulingana na nyumba za baba zao chini ya makamanda wa maelfu, na makamanda wa mamia, naam, Yuda pia, na Benyamini; tangu wenye miaka ishirini na zaidi akawahesabu, akawaona kuwa watu wateule elfu mia tatu, wawezao kwenda vitani, waliozoea mkuki na ngao.


Waovu hukimbia wasipofuatiwa na mtu; Bali wenye haki ni wajasiri kama simba.


Ujiponye kama paa na mkono wa mwindaji, Na kama ndege katika mkono wa mtega mitego.


Ukimbie, mpendwa wangu, Nawe uwe kama paa, au ayala, Juu ya milima ya manukato.


Haya! Pandeni, enyi farasi; Jihimizeni, enyi magari ya vita; Mashujaa nao na watoke nje Kushi na Puti, watumiao ngao; Nao Waludi, washikao uta na kuupinda.


Basi Daudi alikuwa akikaa nyikani ngomeni, akakaa katika nchi ya milima milima kwenye nyika ya Zifu. Naye Sauli alikuwa akimtafuta kila siku, lakini Mungu hakumtia mikononi mwake.


Naye Daudi akakwea kutoka huko, akakaa katika ngome ya Engedi.


Naye Daudi akamwapia Sauli. Kisha Sauli akaenda zake kwao; lakini Daudi na watu wake wakapanda kwenda ngomeni.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo