Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

1 Mambo ya Nyakati 12:40 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

40 Zaidi ya hayo, wale waliokuwa karibu nao, hata mpaka kwa Isakari, na Zabuloni, na Naftali, wakaleta chakula juu ya punda, na ngamia, na nyumbu, na ng'ombe, vyakula vya unga, mikate ya tini, na vichala vya zabibu kavu, na divai, na mafuta, na ng'ombe, na kondoo tele; kwa kuwa kulikuwa na furaha katika Israeli.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

40 Zaidi ya hayo, majirani zao wa karibu na hata wa mbali kama huko Isakari, Zebuluni na Naftali, waliwaletea vyakula walivyobeba kwa punda, ngamia, nyumbu na ng'ombe. Waliwaletea unga, mikate ya tini, vichala vya zabibu kavu, divai na mafuta, ng'ombe na kondoo wengi, kukawa na vyakula tele, kwani kulikuwa na furaha katika Israeli.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

40 Zaidi ya hayo, majirani zao wa karibu na hata wa mbali kama huko Isakari, Zebuluni na Naftali, waliwaletea vyakula walivyobeba kwa punda, ngamia, nyumbu na ng'ombe. Waliwaletea unga, mikate ya tini, vichala vya zabibu kavu, divai na mafuta, ng'ombe na kondoo wengi, kukawa na vyakula tele, kwani kulikuwa na furaha katika Israeli.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

40 Pia, majirani zao hata wale walio mbali hadi Isakari, Zabuloni na Naftali, walikuja wakiwaletea vyakula walivyovibeba kwa punda, ngamia, nyumbu na maksai. Kulikuwa na wingi wa unga, maandazi ya tini, maandazi ya zabibu kavu, divai, mafuta, ng’ombe na kondoo, kwa maana kulikuwa na furaha katika Israeli.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

40 Pia, majirani zao hata wale walio mbali hadi Isakari, Zabuloni na Naftali, walikuja wakiwaletea vyakula walivyovibeba kwa punda, ngamia, nyumbu na maksai. Kulikuwepo na wingi wa unga, maandazi ya tini, maandazi ya zabibu kavu, divai, mafuta, ng’ombe na kondoo, kwa maana kulikuwa na furaha katika Israeli.

Tazama sura Nakili

1 Mambo ya Nyakati 12:40
14 Marejeleo ya Msalaba  

Naye Daudi alipokipita punde hicho kilele cha mlima, tazama, Siba, mtumwa wa Mefiboshethi, akamkuta, na punda wawili waliotandikwa, na juu yao mikate mia mbili ya ngano, na vishada mia moja vya zabibu kavu, na matunda mia moja ya wakati wa joto, na kiriba cha divai.

Kisha watu wote wakapanda juu nyuma yake, watu wakapiga mazomari, wakafurahi kwa shangwe kuu mno, hata nchi ikapasuka kwa sauti zao.

Basi watu wote wa nchi wakafurahi, na mji ukatulia. Naye Athalia wakamwua kwa upanga karibu na nyumba ya mfalme.

Nao walikuwako huko pamoja na Daudi siku tatu, wakila na kunywa; kwani ndugu zao walikuwa wamewaandalia tayari.

Kisha Daudi akafanya shauri na makamanda wa maelfu, na makamanda wa mamia, naam, na kila kiongozi.

wakala na kunywa mbele za BWANA siku ile, kwa furaha kuu. Wakamtawaza Sulemani, mwana wa Daudi, mara ya pili, wakamtia mafuta mbele za BWANA, awe mkuu, na Sadoki awe kuhani.

Wenye haki wasitawipo, mji hufurahi; Waovu wanapoangamia, watu hushangilia.

Wenye haki wakiwa na amri, watu hufurahi; Bali mwovu atawalapo, watu huugua.

BWANA akaniambia, Nenda tena, mpende mwanamke apendwaye na rafiki yake, naye ni mzinzi; kama vile BWANA awapendavyo wana wa Israeli, ingawa wanaigeukia miungu mingine, na kupenda mikate ya zabibu kavu.

Ndipo Abigaili akafanya haraka, akatwaa mikate mia mbili, na viriba viwili vya divai, na kondoo watano waliotayarishwa, na vipimo vitano vya bisi, na vishada mia moja vya zabibu, na mikate ya tini mia mbili; akavipakia vitu hivi juu ya punda.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo