Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Mambo ya Nyakati 12:32 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

32 Na wa wana wa Isakari, watu wenye akili za kujua nyakati, kuyajua yawapasayo Israeli wayatende; vichwa vyao walikuwa watu mia mbili na ndugu zao wote walikuwa chini ya amri yao.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

32 Kutoka kabila la Isakari: Wakuu 200 pamoja na ndugu zao wote waliokuwa chini ya amri yao. Wakuu hao walikuwa na elimu ya kujua mambo ya nyakati na walijua kilichowapasa Waisraeli kufanya.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

32 Kutoka kabila la Isakari: Wakuu 200 pamoja na ndugu zao wote waliokuwa chini ya amri yao. Wakuu hao walikuwa na elimu ya kujua mambo ya nyakati na walijua kilichowapasa Waisraeli kufanya.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

32 Kutoka kabila la Isakari: wakuu 200 pamoja na ndugu zao wote waliokuwa chini ya amri yao. Wakuu hao walikuwa na elimu ya kujua mambo ya nyakati na walijua kilichowapasa Waisraeli kufanya.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

32 Watu wa Isakari, waliofahamu majira na kujua kile ambacho Israeli inapasa kufanya, walikuwa viongozi mia mbili, pamoja na jamaa zao wote chini ya uongozi wao.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

32 Watu wa Isakari, waliofahamu majira na kujua kile ambacho Israeli inapasa kufanya, walikuwa viongozi 200, pamoja na jamaa zao wote chini ya uongozi wao.

Tazama sura Nakili




1 Mambo ya Nyakati 12:32
15 Marejeleo ya Msalaba  

Isakari ni punda hodari, Ajilazaye kati ya mazizi ya kondoo;


Na wa nusu kabila la Manase, elfu kumi na nane, waliotajwa majina yao, ili waje kumtawaza Daudi awe mfalme.


Na pamoja nao, katika vizazi vyao, kulingana na koo za baba zao, walikuwapo vikosi vya jeshi la vita, watu elfu thelathini na sita; kwa kuwa wake zao na watoto wao walikuwa wengi.


Basi mfalme akawaambia wenye hekima, waliojua sheria; maana ndivyo ilivyokuwa desturi ya mfalme kwa wote waliojua sheria na hukumu;


Akili za mwenye busara ni kujua njia yake; Lakini upumbavu wa wapumbavu ni udanganyifu.


Mtu mwenye hekima ana nguvu; Naam, mtu wa maarifa huongeza uwezo;


Hekima ni nguvu zake mwenye hekima, Zaidi ya wakuu kumi waliomo mjini.


Hekima ndiyo bora kupita silaha za vita; Lakini mkosaji mmoja huharibu mema mengi.


Nyakati zako zitakuwa nyakati za kukaa imara; za wokovu tele na hekima na maarifa; kumcha BWANA ni hazina yake ya akiba.


Sauti ya BWANA inaulilia mji, na mtu mwenye akili ataliona jina lako; isikieni hiyo fimbo na yeye aliyeiagiza.


Na asubuhi, mnasema, Leo kutakuwa na dhoruba; kwa maana mbingu ni nyekundu, tena kumetanda. Enyi wanafiki, mnajua kuutambua uso wa mbingu; lakini, je! Ishara za nyakati hizi hamwezi kuzitambua?]


Kwa sababu hiyo msiwe wajinga, bali mfahamu ni nini yaliyo mapenzi ya Bwana.


Mzaliwa wa kwanza wa ng'ombe wake mume, enzi ni yake; Na pembe zake ni pembe za nyati; Kwa hizo atayasukuma mataifa yote, hata ncha za nchi; Nao ni makumi ya maelfu ya Efraimu, Nao ni maelfu ya Manase.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo