Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Mambo ya Nyakati 11:8 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

8 Akaujenga huo mji pande zote, toka Milo na kuuzunguka; naye Yoabu akautengeneza mji uliosalia.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

8 Aliujenga mji huo, akianzia Milo, na kuuzunguka wote, na Yoabu akautengeneza mji huo upya.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

8 Aliujenga mji huo, akianzia Milo, na kuuzunguka wote, na Yoabu akautengeneza mji huo upya.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

8 Aliujenga mji huo, akianzia Milo, na kuuzunguka wote, na Yoabu akautengeneza mji huo upya.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

8 Akajenga mji pande zote, kuanzia Milo hadi kwenye ukuta kuzunguka; wakati huo huo Yoabu akajenga sehemu zingine zilizobaki za Yerusalemu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

8 Akajenga mji pande zote, kuanzia kwenye mito hadi kwenye ukuta kuzunguka, wakati huo huo Yoabu akajenga sehemu zingine zilizobaki za Yerusalemu.

Tazama sura Nakili




1 Mambo ya Nyakati 11:8
8 Marejeleo ya Msalaba  

Na hii ndiyo sababu ya yeye kumwasi mfalme. Sulemani aliijenga Milo, akapafunga palipobomoka pa mji wa baba yake Daudi.


Na hii ndiyo sababu ya shokoa aliyoitoza mfalme Sulemani; ili kuijenga nyumba ya BWANA, na nyumba yake mwenyewe, na Milo, na ukuta wa Yerusalemu, na Hasori, na Megido, na Gezeri.


Nao watumishi wake wakaondoka, wakala njama, wakamwua Yoashi katika nyumba ya Milo, hapo panaposhukia Sila.


Basi Daudi akakaa ngomeni; kwa hiyo ukaitwa mji wa Daudi.


Naye Daudi akaendelea, akazidi kuwa mkuu; kwa maana BWANA wa majeshi alikuwa pamoja naye.


Akanena mbele ya nduguze na mbele ya jeshi la Samaria, akisema, Wayahudi hawa wanyonge wanafanyaje? Je! Watajitengenezea boma? Watatoa dhabihu? Au watamaliza katika siku moja? Je! Watayafufua mawe katika chungu hizi za kifusi, nayo yameteketezwa kwa moto?


lakini ikiwa basi moto na utoke katika Abimeleki na kuwateketeza watu wa Shekemu, na jamaa ya Milo; kisha moto na utoke katika hao watu wa Shekemu, na katika jamaa ya Milo, na kumteketeza Abimeleki.


Kisha hao watu wote wa Shekemu wakakusanyika pamoja, na jamaa yote ya Milo, wakaenda na kumtawaza Abimeleki awe mfalme, karibu na huo mgandi ulio karibu na ngome iliyo katika Shekemu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo