Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Mambo ya Nyakati 11:6 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

6 Naye Daudi akasema, Mtu yeyote atakayekuwa wa kwanza wa kuwapiga Wayebusi, yeye atakuwa mkuu na jemadari. Naye wa kwanza aliyepanda ni Yoabu mwana wa Seruya, naye akawa mkuu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

6 Ndipo Daudi akasema, “Mtu atakayetangulia kuwapiga Wayebusi, atakuwa mkuu na kamanda jeshini.” Basi Yoabu, mwana wa Seruya, akawa wa kwanza kuwashambulia, hivyo akawa mkuu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

6 Ndipo Daudi akasema, “Mtu atakayetangulia kuwapiga Wayebusi, atakuwa mkuu na kamanda jeshini.” Basi Yoabu, mwana wa Seruya, akawa wa kwanza kuwashambulia, hivyo akawa mkuu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

6 Ndipo Daudi akasema, “Mtu atakayetangulia kuwapiga Wayebusi, atakuwa mkuu na kamanda jeshini.” Basi Yoabu, mwana wa Seruya, akawa wa kwanza kuwashambulia, hivyo akawa mkuu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

6 Daudi alikuwa amesema, “Yeyote atakayeongoza mashambulizi dhidi ya Wayebusi atakuwa jemadari mkuu.” Yoabu mwana wa Seruya akawa wa kwanza kukwea, naye akawa mkuu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

6 Daudi alikuwa amesema, “Yeyote aongozaye mashambulizi dhidi ya Wayebusi, atakuwa jemadari mkuu.” Yoabu mwana wa Seruya akawa wa kwanza kukwea, naye akawa mkuu.

Tazama sura Nakili




1 Mambo ya Nyakati 11:6
13 Marejeleo ya Msalaba  

Huyo Yoabu naye, mwana wa Seruya, na watumishi wa Daudi, wakatoka, wakakutana nao karibu na ziwa la Gibeoni; wakaketi, hawa upande huu wa ziwa, na hawa upande huu wa ziwa.


Na wana watatu wa Seruya walikuwako huko, Yoabu, na Abishai, na Asaheli; na Asaheli alikuwa mwepesi wa miguu kama kulungu.


Basi Yoabu alikuwa akiongoza jeshi lote la Israeli; na Benaya, mwana wa Yehoyada, alikuwa akiwaongoza Wakerethi, na Wapelethi;


Basi Abneri alipokuwa amerudi Hebroni, Yoabu akamchukua kando hadi katikati ya lango, ili aseme naye kwa faragha; akampiga mkuki wa tumbo huko, hadi akafa; kwa ajili ya damu ya Asaheli, ndugu yake.


Huyo Yoabu, mwana wa Seruya alikuwa mkuu wa majeshi; na Yehoshafati, mwana wa Ahiludi, mwekaji kumbukumbu;


Akashauriana na Yoabu, mwana wa Seruya, na Abiathari, kuhani; nao wakamsaidia Adonia, wakamfuata.


Na hao wenyeji wa Yebusi wakamwambia Daudi, Hutaingia humu. Walakini Daudi akaitwaa ngome ya Sayuni; huu ndio mji wa Daudi.


Basi Daudi akakaa ngomeni; kwa hiyo ukaitwa mji wa Daudi.


Na Yoabu mwana wa Seruya akawa mkuu wa jeshi; na Yehoshafati mwana wa Ahiludi mwenye kuandika tarehe.


na, baada ya Ahithofeli, walikuwa Yehoyada mwana wa Benaya, na Abiathari; na jemadari wa jeshi la mfalme alikuwa Yoabu.


Ni nani atakayenipeleka hadi mji wenye boma? Ni nani atakayeniongoza hadi Edomu?


Watu wa Israeli wakasema, Je! Mmemwona mtu huyu aliyepanda huko? Hakika ametokea ili awatukane Israeli; basi, itakuwa, mtu yule atakayemwua, mfalme atampa utajiri mwingi, naye atamwoza binti yake, na kuufanya ukoo wa baba yake kuwa huru katika Israeli.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo