Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




1 Mambo ya Nyakati 11:22 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

22 Tena, Benaya, mwana wa Yehoyada, mtu hodari, wa Kabseeli, aliyekuwa amefanya mambo makuu, ndiye aliyewaua simba wakali wawili wa Moabu; pia akashuka, akamwua simba katikati ya shimo wakati wa theluji.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

22 Naye Benaya, mwana wa Yehoyada, kutoka Kabzeeli, alikuwa askari shujaa ambaye alifanya mambo mengi ya ajabu. Aliwaua mashujaa wawili kutoka Moabu, na siku moja wakati wa barafu, alishuka na kuua simba shimoni.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

22 Naye Benaya, mwana wa Yehoyada, kutoka Kabzeeli, alikuwa askari shujaa ambaye alifanya mambo mengi ya ajabu. Aliwaua mashujaa wawili kutoka Moabu, na siku moja wakati wa barafu, alishuka na kuua simba shimoni.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

22 Naye Benaya, mwana wa Yehoyada, kutoka Kabzeeli, alikuwa askari shujaa ambaye alifanya mambo mengi ya ajabu. Aliwaua mashujaa wawili kutoka Moabu, na siku moja wakati wa barafu, alishuka na kuua simba shimoni.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

22 Benaya mwana wa Yehoyada alikuwa mpiganaji hodari kutoka Kabseeli ambaye alifanya mambo makubwa ya ujasiri. Aliwaua mashujaa wawili hodari kuliko wote wa Moabu. Pia alishuka shimoni kulipokuwa na theluji na kumuua simba.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

22 Benaya, mwana wa Yehoyada alikuwa mpiganaji hodari kutoka Kabseeli ambaye alifanya mambo makubwa ya ujasiri. Aliwaua mashujaa wawili waliokuwa hodari kuliko wote wa Moabu. Pia alishuka shimoni kulipokuwa na theluji na kumuua simba.

Tazama sura Nakili




1 Mambo ya Nyakati 11:22
15 Marejeleo ya Msalaba  

Sauli na Yonathani walipendwa na kupendeza Maishani wala mautini hawakutengwa; Walikuwa wepesi kuliko tai, Walikuwa hodari kuliko simba.


Basi Yoabu alikuwa akiongoza jeshi lote la Israeli; na Benaya, mwana wa Yehoyada, alikuwa akiwaongoza Wakerethi, na Wapelethi;


na Benaya, mwana wa Yehoyada, alikuwa juu ya Wakerethi na Wapelethi; nao wana wa Daudi wakawa makuhani.


Basi wakashuka Sadoki, kuhani, na Nathani, nabii, na Benaya, mwana wa Yehoyada, na Wakerethi, na Wapelethi, wakampandisha Sulemani juu ya nyumbu wa mfalme Daudi, wakampeleka mpaka Gihoni.


Ila Sadoki, kuhani, na Benaya, mwana wa Yehoyada, na Nathani, nabii, na Shimei, na Rei, na mashujaa wa Daudi, hao hawakuwa pamoja na Adonia.


Basi Benaya akaja Hemani kwa BWANA, akamwambia, Mfalme asema hivi, Njoo utoke. Naye akajibu, La, sivyo; ila nitakufa papa hapa. Naye Benaya akamletea mfalme habari, akisema, Hivi ndivyo alivyonena Yoabu, na ndivyo alivyonijibu.


Katika wale watatu yeye alikuwa mwenye heshima kuliko hao wawili, akawa kamanda wao; ila hakudiriki kuwamo katika wale watatu.


tena Sadoki, kijana shujaa, na wa nyumba ya babaye, makamanda ishirini na wawili.


Na wa Wagadi wakajitenga kumfuata Daudi ngomeni huko nyikani, wanaume mashujaa, watu waliozoea vita, walioweza kutumia ngao na mkuki; ambao nyuso zao zilikuwa kama nyuso za simba, nao walikuwa wepesi kama kulungu juu ya milima;


Miji ya mwisho ya kabila la wana wa Yuda upande wa kuelekea mpaka wa Edomu katika nchi ya Negebu ilikuwa ni Kabseeli, Ederi, Yaguri;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo