Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

1 Mambo ya Nyakati 11:19 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

19 akasema, Mungu wangu apishe mbali, nisifanye hivi; je! Ninywe damu ya watu hao waliohatarisha nafsi zao? Maana kwa hatari ya nafsi zao wameyaleta. Kwa hiyo hakukubali kuyanywa. Hayo ndiyo waliyoyafanya wale mashujaa watatu.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

19 akisema, “Tendo kama hili lipitishie mbali nami; siwezi kulifanya mbele ya Mungu wangu. Je, waweza kunywa damu ya maisha ya watu hawa? Maana kwa kuyahatarisha maisha yao walileta maji haya.” Kwa hiyo Daudi hakuyanywa maji hayo. Hayo ndio mambo waliyotenda wale mashujaa watatu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

19 akisema, “Tendo kama hili lipitishie mbali nami; siwezi kulifanya mbele ya Mungu wangu. Je, waweza kunywa damu ya maisha ya watu hawa? Maana kwa kuyahatarisha maisha yao walileta maji haya.” Kwa hiyo Daudi hakuyanywa maji hayo. Hayo ndio mambo waliyotenda wale mashujaa watatu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

19 Akasema, “Mungu apishie mbali kwamba nifanye hivi! Je kweli, niinywe damu ya watu hawa waliohatarisha maisha yao?” Kwa sababu walihatarisha maisha yao kuyaleta yale maji, Daudi hakukubali kuyanywa. Huo ndio uliokuwa ujasiri wa wale mashujaa watatu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

1 Mambo ya Nyakati 11:19
16 Marejeleo ya Msalaba  

Bali nyama pamoja na uhai, yaani, damu yake, msile.

Akasema, Hasha, BWANA, nisifanye hivi; je! Si damu hii ya watu hao waliohatarisha nafsi zao? Kwa hiyo hakukubali kuyanywa. Hayo ndiyo waliyoyafanya wale mashujaa watatu.

Nabothi akamwambia Ahabu, BWANA apishe mbali nikupe wewe urithi wa baba zangu.

Basi hao watatu wakapenya jeshi la Wafilisti, wakateka maji kutoka kile kisima cha Bethlehemu, kilicho karibu na lango, wakayachukua, wakamletea Daudi; lakini Daudi hakukubali kuyanywa, akayamimina mbele za BWANA;

Tena Abishai, nduguye Yoabu, alikuwa mkuu wa wale watatu; kwa kuwa aliuinua mkuki wake juu ya watu mia tatu, akawaua; akawa na jina kati ya wale watatu.

Kama watu wa hemani mwangu hawakunena, Ni nani awezaye kumpata mtu asiyeshibishwa na yeye kwa nyama?

Atawakomboa kutoka kwa maonevu na udhalimu, Maana damu yao ina thamani machoni pake.

Kisha mtu yeyote wa nyumba ya Israeli, au miongoni mwa hao wageni wakaao kati yao, atakayekula damu, ya aina yoyote, nitamkataa mtu huyo alaye damu, na nitamtenga na watu wake.

Akawaambia, Hii ndiyo damu yangu ya agano, imwagikayo kwa ajili ya wengi.

Kwa maana mwili wangu ni chakula cha kweli, na damu yangu ni kinywaji cha kweli.

waliokuwa tayari hata kukatwa kichwa kwa ajili ya maisha yangu; ambao ninawashukuru, wala si mimi tu, ila na makanisa ya Mataifa yote pia; nisalimieni na kanisa lililomo katika nyumba yao.

Na sisi, kwa nini tumo hatarini kila saa?

Zabuloni ndio watu waliohatarisha roho zao hadi kufa; Nao Naftali mahali palipoinuka kondeni.

(kwa maana baba yangu aliwatetea ninyi, na kuhatarisha uhai wake, na kuwaokoa na mikono ya Midiani;

Kwa kuwa alihatarisha maisha yake, na kumpiga yule Mfilisti, naye BWANA akawatendea Israeli wote wokovu mkuu. Wewe mwenyewe uliona jambo hilo, ukafurahi; basi kwa nini kukosa juu ya damu isiyo na hatia, umwue huyo Daudi bure?

Tufuate:

Matangazo

Matangazo