Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Mambo ya Nyakati 11:15 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

15 Tena, watatu miongoni mwa wale thelathini waliokuwa wakuu wakashuka mwambani, wakamwendea Daudi, hadi pango la Adulamu; na jeshi la Wafilisti walikuwa wamefanya kambi bondeni mwa Warefai.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

15 Kisha mashujaa watatu kati ya wakuu thelathini waliteremka hadi kwenye mwamba, wakamwendea Daudi kwenye pango huko Adulamu. Wakati huo jeshi la Wafilisti lilikuwa limepiga kambi katika bonde la Refaimu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

15 Kisha mashujaa watatu kati ya wakuu thelathini waliteremka hadi kwenye mwamba, wakamwendea Daudi kwenye pango huko Adulamu. Wakati huo jeshi la Wafilisti lilikuwa limepiga kambi katika bonde la Refaimu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

15 Kisha mashujaa watatu kati ya wakuu thelathini waliteremka hadi kwenye mwamba, wakamwendea Daudi kwenye pango huko Adulamu. Wakati huo jeshi la Wafilisti lilikuwa limepiga kambi katika bonde la Refaimu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

15 Wakuu watatu miongoni mwa wale thelathini walimwendea Daudi kwenye mwamba, katika pango la Adulamu, wakati kikundi cha Wafilisti walikuwa wamepiga kambi katika Bonde la Warefai.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

15 Wakuu watatu miongoni mwa wale thelathini, walimwendea Daudi katika mwamba huko kwenye pango la Adulamu, wakati kikundi cha Wafilisti kilikuwa kimepiga kambi katika Bonde la Warefai.

Tazama sura Nakili




1 Mambo ya Nyakati 11:15
11 Marejeleo ya Msalaba  

Basi Wafilisti walikuwa wamekuja na kujitawanya bondeni mwa Warefai.


Lakini wakapanda hao Wafilisti tena mara ya pili, wakajitawanya bondeni mwa Warefai.


Ndipo hao wakasimama katikati ya shamba lile, wakalipigania, wakawaua Wafilisti; naye BWANA akafanya wokovu mkuu.


na Ishmaya Mgibeoni, shujaa wa wale thelathini, naye alikuwa juu ya wale thelathini; na Yeremia, na Yahazieli, na Yohana, na Yozabadi Mgederathi;


Basi hao Wafilisti walikuwa wamekuja na kujitawanya katika bonde la Warefai.


Tena itakuwa kama hapo mvunaji ashikapo mabua ya ngano, na mkono wake ukatapo masuke; tena itakuwa kama hapo mtu aokotapo masuke katika bonde la Warefai.


Bado, wakazi wa Maresha, nitawaleteeni tena yeye atakayewamiliki; Utukufu wa Israeli utafika Adulamu.


mfalme wa Libna, mmoja; na mfalme wa Adulamu, mmoja;


kisha mpaka ukaendelea karibu na bonde la mwana wa Hinomu, na kufika ubavuni mwa huyu Myebusi upande wa kusini (ndio Yerusalemu); kisha mpaka ukaendelea hata kilele cha mlima ulio pale mkabala wa bonde la Hinomu upande wa magharibi, lililo pale mwisho wa bonde la Warefai upande wa kaskazini;


Basi Daudi akaondoka huko, akakimbilia pango la Adulamu; na ndugu zake na watu wote wa ukoo wa baba yake waliposikia habari hiyo, wakamwendea huko.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo