Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Mambo ya Nyakati 11:14 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

14 Ndipo hao wakasimama katikati ya shamba lile, wakalipigania, wakawaua Wafilisti; naye BWANA akafanya wokovu mkuu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

14 Lakini Daudi na Eliazari walisimama imara katikati ya shamba hilo ili kulitetea, wakawaua Wafilisti; Mwenyezi-Mungu akawaokoa kwa kuwapa ushindi mkubwa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

14 Lakini Daudi na Eliazari walisimama imara katikati ya shamba hilo ili kulitetea, wakawaua Wafilisti; Mwenyezi-Mungu akawaokoa kwa kuwapa ushindi mkubwa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

14 Lakini Daudi na Eliazari walisimama imara katikati ya shamba hilo ili kulitetea, wakawaua Wafilisti; Mwenyezi-Mungu akawaokoa kwa kuwapa ushindi mkubwa.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

14 Lakini Eleazari na Daudi wakasimama imara katikati ya lile shamba, nao wakalishindania na kuwaua Wafilisti. Naye Mwenyezi Mungu akawapa ushindi mkubwa.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

14 Lakini Eleazari na Daudi wakasimama imara katikati ya lile shamba, nao wakalishindania na wakawaua Wafilisti. Naye bwana akawapa ushindi mkubwa.

Tazama sura Nakili




1 Mambo ya Nyakati 11:14
9 Marejeleo ya Msalaba  

huyo aliinuka, akawapiga Wafilisti hata mkono wake ukachoka, na mkono wake ukaambatana na upanga; naye BWANA akafanya wokovu mkuu siku ile; nao watu wakarudi nyuma yake ili kuteka nyara tu.


Basi Naamani, jemadari wa jeshi la mfalme wa Shamu, alikuwa mtu mkubwa mbele ya bwana wake, na mwenye kuheshimiwa, kwa sababu kwa mkono wake BWANA alikuwa amewapa Washami kushinda; tena alikuwa mtu hodari wa vita; lakini alikuwa mwenye ukoma.


Huyo alikuwa pamoja na Daudi huko Pasdamimu; ndiko Wafilisti walikokusanyika vitani, palipokuwa na shamba lililojaa shayiri; na hao watu wakakimbia mbele ya Wafilisti.


Tena, watatu miongoni mwa wale thelathini waliokuwa wakuu wakashuka mwambani, wakamwendea Daudi, hadi pango la Adulamu; na jeshi la Wafilisti walikuwa wamefanya kambi bondeni mwa Warefai.


Awapaye wafalme wokovu, Amwokoa Daudi, mtumishi wake, na upanga wa uovu.


Ampa mfalme wake wokovu mkuu, Amfanyia fadhili masihi wake, Daudi na wazawa wake hata milele.


Farasi huwekwa tayari kwa siku ya vita; Lakini BWANA ndiye aletaye wokovu.


Hivyo BWANA akawaokoa Israeli siku ile; na vita ilienea mpaka kupita Beth-aveni, na watu wote waliokuwa pamoja na Sauli walikuwa kama wanaume elfu kumi. Vita ikanenea katika nchi yenye milima milima ya Efraimu.


Kwa kuwa alihatarisha maisha yake, na kumpiga yule Mfilisti, naye BWANA akawatendea Israeli wote wokovu mkuu. Wewe mwenyewe uliona jambo hilo, ukafurahi; basi kwa nini kukosa juu ya damu isiyo na hatia, umwue huyo Daudi bure?


Tufuate:

Matangazo


Matangazo