Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Mambo ya Nyakati 10:14 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

14 asiulize kwa BWANA; kwa hiyo akamwua, na ufalme akampa Daudi, mwana wa Yese.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

14 badala ya kumwendea Mwenyezi-Mungu ili kumtaka shauri. Kwa sababu hiyo Mwenyezi-Mungu akamuua, na ufalme wake akampa Daudi mwana wa Yese.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

14 badala ya kumwendea Mwenyezi-Mungu ili kumtaka shauri. Kwa sababu hiyo Mwenyezi-Mungu akamuua, na ufalme wake akampa Daudi mwana wa Yese.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

14 badala ya kumwendea Mwenyezi-Mungu ili kumtaka shauri. Kwa sababu hiyo Mwenyezi-Mungu akamuua, na ufalme wake akampa Daudi mwana wa Yese.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

14 hakumuuliza Mwenyezi Mungu. Kwa hiyo Mwenyezi Mungu alimuua, na ufalme akampa Daudi mwana wa Yese.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

14 hakumuuliza bwana. Kwa hiyo bwana alimuua, na ufalme akampa Daudi mwana wa Yese.

Tazama sura Nakili




1 Mambo ya Nyakati 10:14
18 Marejeleo ya Msalaba  

Basi wazee wote wa Israeli wakamwendea mfalme huko Hebroni, naye mfalme Daudi akapatana nao huko Hebroni mbele za BWANA; wakamtia Daudi mafuta awe mfalme juu ya Israeli.


Na hizi ni hesabu za vichwa vya watu wenye silaha za vita, waliokuja Hebroni kwa Daudi, ili kumpa ufalme wa Sauli, sawasawa na neno la BWANA.


Nitakuwa baba yake, naye atakuwa mwanangu; wala sitamwondolea fadhili zangu, kama nilivyomwondolea yeye aliyekuwa kabla yako;


na Boazi akamzaa Obedi; na Obedi akamzaa Yese;


Katika mwaka wa thelathini na tisa wa kumiliki kwake, Asa akashikwa na ugonjwa wa miguu; ugonjwa wake ukazidi sana; lakini hakumtafuta BWANA katika ugonjwa wake, bali alitafuta msaada wa waganga.


Yeye arudishaye mabaya badala ya mema, Mabaya hayataondoka nyumbani mwake.


Je! Shoka lijisifu juu yake alitumiaye? Je! Msumeno ujitukuze juu yake auvutaye? Ingekuwa kana kwamba bakora ingewatikisa waiinuao, au fimbo ingemwinua yeye ambaye si mti.


Lakini hivyo sivyo akusudiavyo mwenyewe, wala sivyo moyo wake uwazavyo; maana katika moyo wake akusudia kuharibu, na kukatilia mbali mataifa, wala si mataifa machache.


Basi wakuu hao wakatwaa katika vyakula vyao, wala wasitake shauri kinywani mwa BWANA.


Lakini sasa ufalme wako hautadumu; BWANA amejitafutia mtu aupendezaye moyo wake, naye BWANA amemwamuru yeye kuwa mkuu juu ya watu wake, kwa sababu wewe hukulishika neno lile BWANA alilokuamuru.


Basi Samweli akamwambia, Leo BWANA amekurarulia ufalme wa Israeli, naye amempa jirani yako, aliye mwema kuliko wewe.


BWANA akamwambia Samweli, utamlilia Sauli hadi lini, kwa kuwa mimi nimemkataa asiwatawale Waisraeli? Ijaze pembe yako mafuta, uende, nami nitakutuma kwa Yese, Mbethlehemi; maana nimejipatia mfalme katika wanawe.


Yeye BWANA amekutendea kama alivyosema kwa kinywa changu; BWANA amekurarulia ufalme mkononi mwako, na kumpa jirani yako, yaani, Daudi.


Lakini Sauli alipouliza kwa BWANA, BWANA hakumjibu, wala kwa ndoto, wala kwa Urimu, wala kwa manabii.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo