Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yuda 1:4 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

4 Kwa maana kuna watu wamejiingiza kwa siri, watu walioandikiwa zamani hukumu hii, makafiri, wabadilio neema ya Mungu wetu kuwa ufasiki, nao humkana yeye aliye peke yake Mola, na Bwana wetu Yesu Kristo.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

4 Maana watu wasiomcha Mungu wamepata kujiingiza kwa siri miongoni mwetu, watu ambao, kwa faida ya maisha yao mabaya, wanaupotosha ujumbe wa neema ya Mungu wetu na kumkana Yesu Kristo aliye peke yake Kiongozi na Bwana wetu. Lakini, Maandiko Matakatifu yalikwisha bashiri tangu zamani hukumu inayowangojea watu hao.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

4 Maana watu wasiomcha Mungu wamepata kujiingiza kwa siri miongoni mwetu, watu ambao, kwa faida ya maisha yao mabaya, wanaupotosha ujumbe wa neema ya Mungu wetu na kumkana Yesu Kristo aliye peke yake Kiongozi na Bwana wetu. Lakini, Maandiko Matakatifu yalikwisha bashiri tangu zamani hukumu inayowangojea watu hao.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

4 Maana watu wasiomcha Mungu wamepata kujiingiza kwa siri miongoni mwetu, watu ambao, kwa faida ya maisha yao mabaya, wanaupotosha ujumbe wa neema ya Mungu wetu na kumkana Yesu Kristo aliye peke yake Kiongozi na Bwana wetu. Lakini, Maandiko Matakatifu yalikwisha bashiri tangu zamani hukumu inayowangojea watu hao.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

4 Kwa kuwa kuna watu waliojipenyeza kwa siri kati yenu, watu walioandikiwa tangu zamani hukumu hii, waovu, wanaopotosha neema ya Mungu, na kuifanya kuwa ruhusa ya kutenda maovu, wakimkana Isa Al-Masihi, ambaye pekee ni Mtawala wetu mkuu na Bwana wetu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

4 Kwa kuwa kuna watu waliojipenyeza kwa siri katikati yenu, watu walioandikiwa tangu zamani hukumu hii, waovu, wapotoshao neema ya Mungu wetu kuwa ufisadi wakimkana yeye aliye Bwana wetu wa pekee, Bwana Isa Al-Masihi.

Tazama sura Nakili




Yuda 1:4
32 Marejeleo ya Msalaba  

lakini watu walipolala, akaja adui yake akapanda magugu katikati ya nganu, akaenda zake.


Na uzima wa milele ni huu, wakujue wewe, Mungu wa peke yake, wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma.


Nae, alipokwisha kufika na kuiona neema ya Mungu akafurahi, akawasihi wote waambatane na Bwana kwa kusudi la moyo.


Kwa kuwa tumesikia ya kwamba watu waliotoka kwetu wamewasumbueni kwa maneno yao, wakipotosha roho zenu, wakisema, ya kuwa hamna buddi kutahiriwa na kuishika Torati, ambao sisi hatukuwapa agizo lo lote;


bali kwa ajili ya ndugu za uwongo walioingizwa kwa siri.


Maana ninyi, ndugu, mliitwa mpate uhuru; lakini uhuru wenu usiwe sababu ya kuufuata mwili, bali khudumianeni kwa upendo.


illi tusiwe tena watoto wachanga, tukitupwa huku na huku, na kuchukulivva kwa killa upepo wa elimu, kwa bila ya watu, kwa ujanja, tukifuata njia za udanganyifu;


Lakini mtu asiyewatunza walio wake na khassa watu wa nyumba yake ameikana Imani, tena ni mbaya kuliko yeye asiyeamini.


kama tukistahimili, tutamiliki pamoja nae pia; kama tukimkana yeye, yeye nae atatukana sisi:


Kwa maana katika hawa wamo wale wajiingizao kalika nyumba za watu, na kuchukua mateka wanawake wajinga wenye mizigo ya dhambi, waliochukuliwa na tamaa za namna nyingi,


kama huru, na wasiontumia uhuru kwa kusetiri ubaya, bali kaina watumwa wa Mungu.


tena, Jiwe lakujikwaza mguu, na mwamba wa kujiangusha; maana hujikwaza kwa neno lile, wakiliasi, nao waliwekwa wapate hayo.


Na mwenye haki akiokoka kwa shidda, yule asiyemcha Mungu na mwenye dhambi ataonekana wapi?


na khassa wale waufuatao mwili katika tamaa ya mambo machafu, na kudharau mamlaka. Wenye ushupavu, wenye kujikinai, hawatetemeki wakiyatukana matukufu;


akamwokoa Lut, aliyehuzunishwa na mwenendo wa uasharati wa hawo wakhalifu;


Lakini mbingu za sasa na inchi zimewekwa akiba kwa moto, kwa neno lilo hilo, zikilindwa hatta siku ya hukumu, na ya kuangamia kwao wana Adamn wasiomcha Mungu.


Naui aliye mwongo illa yeye akanae ya kuwa Yesu ni Kristo? Huyo ndiye adui wa Kristo, amkanae Baba na Mwana.


illi afanye hukumu juu ya waiu wote, na kuwaadhibisha wote wasiomcha Mungu, kwa ajili ya kazi zao zote walizoziteuda bila kumcha Mungu, na kwa ajili ya maneno magumu yote ambayo hawo wenye dhambi wasiomcha Mungu wameyanena juu yake.


ya kwamba waliwaambia ya kuwa wakati wa mwisho watakuwuko watu wenye kudhihaki, wakizifuata tamaa zao wenyewe zilizo kinyume cha mapenzi ya Mungu.


Ni nani asiyekucha, Bwana, na kulitukuza jina lako? kwa kuwa wewe peke yako Mtakatifu: kwa maana mataifa yote watakuja na kusujudu mbele yako; kwa kuwa matendo yako ya haki yamekwisha kufunuliwa.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo