Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yuda 1:25 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

25 Yeye aliye Mungu pekee, mwenye hekima, Mwokozi wetu: kwake yeye utukufu, na ukuu, na uwezo, na nguvu kwa Yesu Kristo, tangu milele, na sasa, na hatta milele. Amin.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

25 kwake yeye aliye peke yake Mungu, Mkombozi wetu, uwe utukufu, ukuu, nguvu na mamlaka kwa njia ya Kristo Bwana wetu, tangu zama zote, sasa na hata milele! Amina.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

25 kwake yeye aliye peke yake Mungu, Mkombozi wetu, uwe utukufu, ukuu, nguvu na mamlaka kwa njia ya Kristo Bwana wetu, tangu zama zote, sasa na hata milele! Amina.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

25 kwake yeye aliye peke yake Mungu, Mkombozi wetu, uwe utukufu, ukuu, nguvu na mamlaka kwa njia ya Kristo Bwana wetu, tangu zama zote, sasa na hata milele! Amina.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

25 kwake yeye Mungu pekee Mwokozi wetu, kwa Isa Al-Masihi Bwana wetu, utukufu, ukuu, uweza na mamlaka ni vyake tangu milele, sasa na hata milele! Amen.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

25 kwake yeye Mungu pekee Mwokozi wetu, kwa Isa Al-Masihi Bwana wetu, utukufu, ukuu, uweza na mamlaka ni vyake tangu milele, sasa na hata milele! Amen.

Tazama sura Nakili




Yuda 1:25
32 Marejeleo ya Msalaba  

Usitutie majaribuni, bali utuokoe na yule mwovu.


Roho yangu yamfurahia Mungu, Mwokozi wangu.


Ninyi mnaabudu msichokijua; sisi tunaabudu tukijuacho: kwa kuwa wokofu watoka kwa Wayahudi.


Mwawezaje kuamini ninyi mnaopokezanya utukufu ninyi kwa ninyi, na utukufu ule utokao kwa Mungu aliye wa pekee hamwutafuti?


Ee ajabu ya utajiri na hekima na maarifa ya Mungu; hazina hatta kiasi! hukumu zake hazichunguziki, na njia zake hazitafutikani!


Kwa maana vitu vyote vyatoka kwake, viko kwa uweza wake, vinarejea kwake. Utukufu una yeye milele. Amin.


yeye ndiye Mungu mwenye hekima peke yake; na atukuzwe kwa Yesu Kristo, milele na milele. Amin.


aliyotuzidishia katika hekima yote na ujuzi;


illi sasa, kwa njia ya kanisa, hekima ya Mungu iliyo ya namna nyingi ijulikane na falme na mamlaka ya mbinguni;


kwake yeye utukufu katika Kanisa, na katika Kristo Yesu hatta vizazi vyote vya milele na milele. Amin.


Kwa Mfalme wa milele, asiyeweza kuona uharibifu, asiyeonekana, Mungu wa hekima peke yake, kwake yeye heshima na utukufu milele na milele. Amin.


Maana hili ni zuri, lenye kibali mbele za Mwokozi wetu Mungu


wasiwe waibaji, bali wakionyesha uaminifu mwema wote, illi wayapambe mafundisho ya Mwokozi wetu katika mambo yote.


tukilitazamia tumaini lenye baraka na mafunuo ya utukufu wa Mungu mkuu, Mwokozi wetu Yesu Kristo;


Lakini wenia wa Mwokozi wetu Mungu na upendo wake kwa wana Adamu ulipoonekana,


Yesu Kristo, jana na leo yeye yule na hatta milele.


Mtu akisema, na aseme kama mausia ya Mungu; mtu akikhudumu, na akhudumu kwa nguvu anazojaliwa na Mungu; illi Mungu atukuzwe katika mambo yote kwa Yesu Kristo; utukufu na uweza u kwake hatta milele na milele. Amin.


SIMON PETRO, mtumwa na mtume wa Yesu m Kristo, kwao waiiopata imani moja na sisi, yenye thamani, katika haki ya Mungu wetu, na Mwokozi wetu Yesu Kristo.


Lakini, kaeni katika neema, na katika kumjua Bwana wetu, Mwokozi wetu, Yesu Kristo. Utukufu una yeye sasa na hatta milele. Amin.


na kutufanya kuwa ufalme, na makuhani kwa Mungu, Baba yake: utukufu na ukuu una Yeye hatta milele na milele. Amin.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo