Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yuda 1:21 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

21 jilindeni katika upendo wa Mungu, mkingojea rehema ya Bwana wetu Yesu Krislo, hatta mpate uzima wa milele.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

21 na kudumu katika upendo wa Mungu, mkimngojea Bwana wetu Yesu Kristo ambaye, kwa huruma yake, atawajalieni uhai wa milele.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

21 na kudumu katika upendo wa Mungu, mkimngojea Bwana wetu Yesu Kristo ambaye, kwa huruma yake, atawajalieni uhai wa milele.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

21 na kudumu katika upendo wa Mungu, mkimngojea Bwana wetu Yesu Kristo ambaye, kwa huruma yake, atawajalieni uhai wa milele.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

21 Jilindeni katika upendo wa Mungu mkitazamia rehema ya Bwana wetu Isa Al-Masihi, inayowapeleka katika uzima wa milele.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

21 Jilindeni katika upendo wa Mungu mkitazamia kwa furaha rehema ya Bwana wetu Isa Al-Masihi ili awalete katika uzima wa milele.

Tazama sura Nakili




Yuda 1:21
31 Marejeleo ya Msalaba  

Kwa kuwa torati ilitolewa kwa mkono wa Musa, neema na kweli zilikuwa kwa mkono wa Yesu Kristo.


Aliye na amri zangu, na kuzishika, yeye ndiye anipendae; nae anipendae atapendwa na Baba yangu, nami nitampenda, na kujidhihirisha kwake.


Nae, alipokwisha kufika na kuiona neema ya Mungu akafurahi, akawasihi wote waambatane na Bwana kwa kusudi la moyo.


illi, kama vile dhambi ilivyotawaia katika mauti, vivyo hivyo kwa njia ya haki neema itawale hatta uzima wa milele kwa Yesu Kristo Bwana wetu.


na tumaini halitahayarishi, kwa maana pendo la Mungu limekwisha kumiminwa katika mioyo yetu na Roho Mtakatifu tuliyepcwa sisi.


Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; hali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.


wala yaliyo juu, wala yaliyo chini, wala kiumbe cho chote kinginecho hakitaweza kututenga na upendo wa Mungu ulio katika Yesu Kristo Bwana wetu.


Neema ya Bwana Yesu Kristo, na pendo la Mungu, na ushirika wa Roho Mtakatifu ukae nanyi nyote. Amin.


Bwana awaongozeni mioyo yenu mkapate pendo la Mungu, na uvumilivu wa Kristo.


kwa Timotheo, mwana wangu khassa katika imani, Neema, na rehema, na amani zitokazo kwa Mungu Baba na kwa Kristo Yesu Bwana wetu.


Bwana awape rehema walio wa uyumba ya Onesiforo; maana marra nyingi aliniburudisha, wala hakuutahayarikia mnyororo wangu;


Bwana na ampe kuona rehema kwa Bwana siku ile. Na jinsi alivyonikhudumia katika Efeso, wewe wajua sana.


kwa Timotheo mwanangu mpendwa; Neema, na rehema, na amani, zitokazo kwa Mungu Baba na kwa Kristo Yesu Bwana wetu.


baada ya haya nimewekewa taji ya baki, ambayo Bwana mhukumu wa haki atanipa katika siku ile: wala si mimi tu, bali watu wote pia waliopenda kutokea kwake.


kadhalika Kristo, akiisha kutolewa sadaka marra moja aziondoe dhambi za watu wengi, marra ya pili, pasipo dhambi, ataonekana nao wamtazamiao kwa wokofu.


mkitazamia hatta ije siku ile ya Mungu, na kuihimiza; ambayo katika hiyo mbingu zitafumuliwa zikiungua, na viumbe vya asili vitateketea na kuyeyuka.


Na sisi tumelifahamu pendo alilo nalo Mungu ndani yetu na kuliamini. Mungu ni pendo, nae akaae katika pendo, hukaa ndani ya Mungu, na Mungu hukaa ndani yake.


Twajua ya kuwa killa mtu aliyezaliwa na Mungu hakosi: bali yeye aliyezaliwa na Mungu ajilinda, na yule mwovu hamgusi.


Watoto wangu wadogo, jilindeni nafsi zenu na sanamu.


YUDA, mtumwa wa Yesu Kristo, ndugu wa Yakobo, kwao waliopendwa katika Mungu Baba, na kuhifadhiwa kwa ajili ya Yesu Kristo baada ya kuitwa;


Wahurumiane wengine walio na mashaka;


Kwake Yeye awezae kuwalinda ninyi msijikwae, na kuwasimamisha mbele ya utukufu wake bila mawaa katika furaha kuu,


Nao wakamshinda kwa damu ya Mwana kondoo, na kwa neno la ushuhuda wao; wala hawakupenda maisha yao hatta wakati wa kufa.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo