Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yuda 1:16 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

16 Watu hawa ni wenye kunungʼunika, wenye kulalamika, waendao kwa tamaa zao, na vinywa vyao vyanena maneno ya kiburi makuu mno, wakipendelea watu wenye cheo kwa ajili ya faida.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

16 Watu hawa hunung'unika daima, hulalamika, hufuata tamaa zao mbaya, hujigamba na kuwasifu watu wengine mno kwa faida yao wenyewe.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

16 Watu hawa hunung'unika daima, hulalamika, hufuata tamaa zao mbaya, hujigamba na kuwasifu watu wengine mno kwa faida yao wenyewe.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

16 Watu hawa hunung'unika daima, hulalamika, hufuata tamaa zao mbaya, hujigamba na kuwasifu watu wengine mno kwa faida yao wenyewe.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

16 Watu hawa ni wenye kunung’unika na wenye kutafuta makosa; wao hufuata tamaa zao mbovu; hujisifu kwa maneno makuu, na kuwasifu mno watu wengine kwa faida yao wenyewe.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

16 Watu hawa ni wenye kunung’unika na wenye kutafuta makosa; wao hufuata tamaa zao mbaya, hujisifu kwa maneno makuu kuhusu wao wenyewe na kuwasifu mno watu wenye vyeo kwa ajili ya kujipatia faida.

Tazama sura Nakili




Yuda 1:16
38 Marejeleo ya Msalaba  

Mafarisayo na wandishi wakanungʼunika, wakasema, Huyu hukaribisha wenye dhambi, hula pamoja nao.


Hatta watu walipoona wakanungʼunika wote, wakisema, ya kama, Ameingia akae kwa mtu mwenye dhambi.


Mafarisayo na waandishi wao wakawanungʼunikia wanafunzi wake, wakisema, Kwa nini mnakula na kunywa pamoja na watoza ushuru na wenye dhambi?


Bassi Wayahudi wakamnungʼunikia, kwa sababu alisema, Mimi ni mkate ulioshuka kutoka mbinguni.


Yesu akajua nafsini mwake ya kuwa wanafunzi wake wanaliumigʼunikia neno hili, akawaambia, Neno hili linawachukiza?


Wala msinungʼunike, kama wengine wao walivyommgʼunika, wakaharibiwa na mharabu.


Nasema, Enendeni kwa Roho, nanyi hamtatimiza tamaa za mwili.


Nao walio watu wa Kristo Yesu wameusulibisha niwili pamoja na mawazo mabaya na tamaa mbaya.


Yatendeni mambo yote pasipo manungʼuniko na mashindano,


si katika hali ya tamaa mbaya, kama mataifa wasiomjua Mungu;


na majadiliano ya watu walioharibiwa akili zao, walioikosa kweli, wakidhani ya kuwa utawa ni njia ya kupata faida; ujitenge na watu kama hao,


Maana ntakuja wakati watakapoikataa elimu yenye uzima; bali kwa kuzifuata nia zao wenyewe watajipatia waalimu makundi makundi, kwa kuwa wana masikio ya utafiti,


Kama watoto wa kutii msijifananishe na tamaa zenu za kwanza, za ujinga wenu;


Mapenzi, nakusihini kama wapitaji na wasafiri, ziepukeni tamaa za mwili zipiganazo na roho;


kuanzia sasa tusiendelee kuishi katika tamaa za wana Adamu, bali katika mapenzi ya Mungu, wakati wetu wa kukaa hapa duniani uliobakia.


na khassa wale waufuatao mwili katika tamaa ya mambo machafu, na kudharau mamlaka. Wenye ushupavu, wenye kujikinai, hawatetemeki wakiyatukana matukufu;


wakinena maneno ya kiburi makuu mno, kwa tamaaza mwili na kwa uasharati huwakhadaa watu waliokwisha kuwakimbia wao waishio katika udanganyifu:


Mkijua kwanza neno hili ya kwamba katika siku za mwisho watakuja watu wenye kudhihaki, wafuatao tamaa zao wenyewe,


illi afanye hukumu juu ya waiu wote, na kuwaadhibisha wote wasiomcha Mungu, kwa ajili ya kazi zao zote walizoziteuda bila kumcha Mungu, na kwa ajili ya maneno magumu yote ambayo hawo wenye dhambi wasiomcha Mungu wameyanena juu yake.


ya kwamba waliwaambia ya kuwa wakati wa mwisho watakuwuko watu wenye kudhihaki, wakizifuata tamaa zao wenyewe zilizo kinyume cha mapenzi ya Mungu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo