Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yuda 1:14 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

14 Na Enok, wa saba baada ya Adamu, alitoa maneno ya unabii juu ya hawo, akisema, Angalia, Bwana alikuja na elfu kumi za watakatifu wake,

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

14 Naye Henoki, ambaye ni babu wa saba tangu Adamu, alibashiri hivi juu ya watu hao: “Sikilizeni! Bwana anakuja pamoja na maelfu ya malaika wake watakatifu

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

14 Naye Henoki, ambaye ni babu wa saba tangu Adamu, alibashiri hivi juu ya watu hao: “Sikilizeni! Bwana anakuja pamoja na maelfu ya malaika wake watakatifu

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

14 Naye Henoki, ambaye ni babu wa saba tangu Adamu, alibashiri hivi juu ya watu hao: “Sikilizeni! Bwana anakuja pamoja na maelfu ya malaika wake watakatifu

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

14 Idrisi, mtu wa saba kuanzia Adamu, alitoa unabii kuhusu watu hawa, akisema: “Tazama, Mwenyezi Mungu anakuja pamoja na maelfu kwa maelfu ya watakatifu wake,

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

14 Idrisi, mtu wa saba kuanzia Adamu alitoa unabii kuhusu watu hawa, akisema: “Tazama, Mwenyezi Mungu anakuja pamoja na maelfu kwa maelfu ya watakatifu wake,

Tazama sura Nakili




Yuda 1:14
18 Marejeleo ya Msalaba  

Kwa maana Mwana wa Adamu atakuja katika utukufu wa Baba yake pamoja na malaika zake; ndipo atamlipa killa mtu kwa kadiri ya kutenda kwake.


Hatta atakapokuja Mwana wa Adamu katika utukufu wake, na malaika watakatifu wote pamoja nae, ndipo atakapoketi katika kiti cha utukufu wake:


apate kuifanya imara mioyo yenu iwe bila lawama katika utakatifu mbele za Mungu, Baba yetu, wakati wa kuja kwake Bwaua wetu Yesu pamoja na watakatifu wake wote.


Bali ninyi mmeufikilia mlima Sayuni, na mji wa Mungu aliye tiayi, Yerusalemi wa mbinguni, na majeshi ya malaika elfu nyingi,


Tazama yuaja na mawingu: na killa jicho litamwona, na hawo waliomchoma; na kabila zote za dunia wataomboleza kwa ajili yake. Naam. Amin.


Nikaona, nikasikia sauti ya malaika wengi pande zote za kile kiti cha enzi, na za wale nyama wenye uhayi, na za wale wazee, na hesabu yao, elfu kumi marra elfu kumi, na elfu marra elfu,


Tufuate:

Matangazo


Matangazo