Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Yuda 1:12 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

12 Watu hawa ni miamba yenye khatari katika karamu zenu za upendo wafanyapo karamu pamoja nanyi, wakijilisha pasipo khofu; ni mawingu yasiyo na maji, yachukuliwayo na upepo; ni miti iliyopukutika, isiyo na matunda, iliyokufa marra mbili, na kungʼolewa kabisa;

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

12 Kwa makelele yao yasiyo na adabu, na kwa kujipendelea wao wenyewe, watu hao ni kama madoa machafu kwenye karamu mnazoshiriki kwa upendo. Wako kama mawingu yasiyo na mvua yanayopeperushwa na upepo. Wao ni kama miti iliyopukutika isiyozaa matunda, iliyokufa kabisa, iliyong'olewa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

12 Kwa makelele yao yasiyo na adabu, na kwa kujipendelea wao wenyewe, watu hao ni kama madoa machafu kwenye karamu mnazoshiriki kwa upendo. Wako kama mawingu yasiyo na mvua yanayopeperushwa na upepo. Wao ni kama miti iliyopukutika isiyozaa matunda, iliyokufa kabisa, iliyong'olewa.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

12 Watu hawa ni dosari katika karamu zenu za upendo, wakila pamoja nanyi bila hofu, wakijilisha wenyewe tu. Wao ni mawingu yasiyokuwa na maji, yakichukuliwa na upepo, miti isiyo na matunda wakati wa mapukutiko, ambayo hunyauka, iliyokufa mara mbili na kung’olewa kabisa.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

12 Watu hawa ni dosari katika karamu zenu za upendo, wakila pamoja nanyi bila hofu, wakijilisha pasipo hofu. Wao ni mawingu yasiyokuwa na maji, yakichukuliwa na upepo, miti isiyo na matunda wakati wa mapukutiko, ambayo hunyauka, iliyokufa mara mbili na kung’olewa kabisa.

Tazama sura Nakili

Yuda 1:12
35 Marejeleo ya Msalaba  

na jua lilipozuka zikanyauka; na kwa kuwa hazina mizizi zikakauka.

Akajibu, akasema, Killa pando asilolipanda Baba yangu wa mbinguni, litangʼolewa.

hatta jua lilipoznka zikaungua, na kwa kuwa hazina mizizi zikakauka.

Bali mtumwa yule akisema moyoni mwake, Bwana wangu anakawia kuja; akaanza kuwapiga wajoli wake, wanaume na wanawake, na kula na kulewa;

Palikuwa na mtu tajiri, aliyevaa porfuro na bafuta, akafanya furaha kilia siku na anasa.

Bassi, jiangalieni, mioyo yenu isije ikalemewa na ulafi na ulevi, na masumbufu ya maisha haya,

Nyingine zikaanguka penye mwamba, zikamea, zikakauka kwa kukosa maji.

illi tusiwe tena watoto wachanga, tukitupwa huku na huku, na kuchukulivva kwa killa upepo wa elimu, kwa bila ya watu, kwa ujanja, tukifuata njia za udanganyifu;

mwisho wao uharibifu, mungu wao tumbo, utukufu wao u katika aibu yao, waniao mambo ya duniani.

Na yeye asiyejizuia nafsi yake amekufa ingawa yu hayi.

Msichukuliwe na mafundisho ya namna nyingine nyingine, na ya kigeni; maana ni vizuri moyo ufanywe imara kwa neema, wala si kwa vyakula, ambavyo wao waliokwenda navyo bawakupata faida.

Mmefanya anasa katika dunia, na kujifurahisha kwa tamaa; mmejilisha mioyo yenu kama siku ya machinjo.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo