Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yohana 9:39 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

39 Yesu akasema, Mimi nimekuja ulimwenguni humu kwa hukumu, illi wasioona waone, nao wanaoona wawe vipofu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

39 Yesu akasema, “Mimi nimekuja ulimwenguni kutoa hukumu, kusudi wasioona wapate kuona, na wale wanaoona wawe vipofu.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

39 Yesu akasema, “Mimi nimekuja ulimwenguni kutoa hukumu, kusudi wasioona wapate kuona, na wale wanaoona wawe vipofu.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

39 Yesu akasema, “Mimi nimekuja ulimwenguni kutoa hukumu, kusudi wasioona wapate kuona, na wale wanaoona wawe vipofu.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

39 Isa akasema, “Nimekuja ulimwenguni humu kwa ajili ya kuhukumu, ili wale walio vipofu wapate kuona, nao wale wanaoona wawe vipofu.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

39 Isa akasema, “Nimekuja ulimwenguni humu kwa ajili ya kuhukumu, ili wale walio vipofu wapate kuona, nao wale wanaoona, wawe vipofu.”

Tazama sura Nakili




Yohana 9:39
34 Marejeleo ya Msalaba  

vipofu wanapata kuona, viwete wanatembea, wenye ukoma wanatakasika, viziwi wanasikia, wafu wanafufuliwa, na maskini wanakhubiriwa khabari njema.


Waacheni hawo; ni vipofu, viongozi wa vipofu. Na kipofu akimwongoza kipofu mwenzake, watatumhukia shimoni wote wawili.


Lakini jicho lako likiwa ovu, mwili wako wote utakuwa na giza. Bassi ile nuru iliyomo ndani yako ikiwa giza, giza gani hilo!


Kuwaangaza wakaao katika giza na uvuli wa mauti, Na kuelekeza miguu yetu mnamo njia ya amani.


Kafahamuni, wako wa mwisho watakaokuwa wa kwanza, na wako wa kwanza watakaokuwa wa mwisho.


Sumeon akawabariki, akamwambia Mariamu, mama yake, Hakika huyu amewekwa, waanguke, wasimame wengi katika Israeli; awe ishara inenwayo;


Roho ya Bwana ni juu yangu, Kwa sababu amenitia mafuia kuwakhubiri maskini khabari njema. Amenituma kuwaponya waliopondeka moyo, Kuwatangazia wafungwa kufunguliwa, na vipofu kupata kuona tena, Kuwaacha wa huru waliosetwa,


Saa ileile akawaponya watu wengi maradhi zao, na misiba yao, na pepo wabaya: na vipofu wengi akawakarimia kuona.


Sasa hukumu ya ulimwengu huu ipo, sasa mkuu wa ulimwengu him atatupwa nje.


Mimi nimekuja niwe nuru ulimwenguni, illi kilia aniaminiye mimi asikae gizani.


Maana Mungu hakumpeleka Mwana wake ulimwenguni auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe nae.


Na hii ndiyo hukumu, ya kuwa nuru imekuja ulimwenguni, watu wakapenda giza zaidi ya nuru; kwa maana matendo yao yalikuwa maovu.


Bassi Yesu akanena nao tena, akisema. Mimi ni nuru ya ulimwengu; anifuatae hatakwenda katika giza kamwe, bali atakuwa na nuru ya uzima.


Ninyi mwahukumu kwa jinsi ya kiwiliwili; mimi simhukumu mtu.


Bassi yule mtu akajibu akasema, Kwamba yeye m mwenye dhambi, sijui. Najua neno moja, mimi nalikuwa kipofu, na sasa naona.


uwafumhue macho yao, waiache giza na kuielekea nuru, na waziache nguvu za Shetani na kumwelekea Mungu, na wapate masamaha ya dhambi zao, na urithi miongoni mwao waliotakaswa kwa imani iliyo kwangu.


katika hao wa kwanza manukato ya mauti yao waendao hatta mauti; katika hao wengine manukato ya uzima wao waendao hatta uzima. Na nani atoshae kwa mambo haya?


Kwa biyo anena, Amka, wewe usinziae, kafufuka, na Kristo atakuangaza.


na katika madanganya yote ya udhalimu kwao wanaopotea: kwa sababu hawakukubali kuipenda kweli, wapate kuokolewa.


Bali ninyi m mzao mteule, ukubani wa kifaume, taifa takatifu, watu wa milki, mpate kutangaza fadhili zake aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu;


Bali yeye amchukiae ndugu yake, yu katika giza, tena anakwenda katika giza, wala hajui aendako, kwa sababu giza imempofusha macho.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo