Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yohana 9:34 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

34 Wakajibu, wakamwambia, Wewe ulizaliwa katika dhambi tupu, nawe unatufuudisha sisi? Wakamtoa nje.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

34 Wao wakamjibu, “Wewe ulizaliwa na kulelewa katika dhambi; unawezaje kutufundisha sisi?” Basi, wakamfukuza sunagogini.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

34 Wao wakamjibu, “Wewe ulizaliwa na kulelewa katika dhambi; unawezaje kutufundisha sisi?” Basi, wakamfukuza sunagogini.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

34 Wao wakamjibu, “Wewe ulizaliwa na kulelewa katika dhambi; unawezaje kutufundisha sisi?” Basi, wakamfukuza sunagogini.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

34 Wakamjibu, “Wewe ulizaliwa katika dhambi kabisa, nawe unajaribu kutufundisha?” Wakamfukuza atoke nje.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

34 Wao wakamjibu, “Wewe ulizaliwa katika dhambi kabisa, nawe unajaribu kutufundisha?” Wakamfukuza atoke nje.

Tazama sura Nakili




Yohana 9:34
34 Marejeleo ya Msalaba  

Mtu mmoja katika wana sharia akajibu, akamwambia, Mwalimu, ukisema haya watushutumu sisi nasi.


Kwa maana killa ajikwezae atadhilika; nae ajidhiliye atakwezwa.


Amin, nawaambieni, Yeye yote asiyeukubali ufalme wa Mungu kama mtoto, hatauingia kamwe.


M kheri ninyi, wana Adamu watakapowachukieni na watakapowaharamisha, na kuwashutumu, na kulitupa nje jina lenu kuma kitu kiovu, kwa ajili yake Mwana wa Adamu.


Yote anipayo Bwana itakuja kwangu; nae ajae kwangu sitamtupa nje kamwe.


Wakamwambia, Sisi hatukuzaliwa kwa zina; tuna baba mmoja, yaani Mungu.


Wanafunzi wake wakamwuliza, wakinena, Rabbi, ni nani aliyetenda dhambi, mtu huyu au wazazi wake, hatta akazaliwa kipofu?


Wazazi wake waliyasema haya kwa sababu waliwaogopa Wayahudi; kwa maana Wayahudi wamekwisha kuwafikana kwamba mtu akimwungama kuwa Kristo, ataharamishwa sunagogi.


Yesu akasikia kwamba wamemtoa nje; akamwona, akasema, Wewe wamwamini Mwana wa Mungu?


Baadhi ya Mafarisayo waliokuwa pamoja nae wakasikia haya, wakamwambia, Je! sisi nasi tu vipofu?


Bali hao walio nje Mungu atawahukumu. Mwondoeni mtu yule mbaya, asikae kwenu.


Sisi tulio Wayahudi kwa asili, wala si wenye dhambi wa mataifa,


ambazo sisi nasi sote tuliziendea, hapo zamani, katika tamaa za mwili wetu, tukiyatimiza mapenzi ya mwili wetu na ya nia zetu, tukawa kwa tabia yetu watoto wa ghadhabu kama na hao wengine.


Vivyo hivyo ninyi vijana, watiini wazee. Naam, ninyi nyote jifungeni unyenyekevu kama mshipi, mpate kukhudumiana; kwa sababu Mungu hushindana na wenye kiburi, huwapa wanyenyekevu neema.


Kwa hiyo, nikija, nitamkumbusha matendo yake ate-ndayo, akitoa upuzi juu yetu kwa maneno maovu; wala hatoshwi na hayo, yeye mwenyewe hawakaribishi ndugu, na wale watakao kuwakaribisha, huwazuia, na kuwatoa katika kanisa.


Naliliandikia kanisa, lakini Diotrefe apendae kuwa wa kwanza kati yao, hatukubali.


tena kwamba mtu aliye yote asimmne wala kuuza, isipokuwa ana alama ile au jimi la nyama yule, au hesabu ya jina lake.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo