Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yohana 9:30 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

30 Yule mtu akajibu akawaambia, Neno hili ni la ajabu, kwamba ninyi hamjui atokako, nae alinifumbua macho.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

30 Naye akawajibu, “Hili ni jambo la kushangaza! Nyinyi hamjui ametoka wapi, lakini amenifumbua macho yangu!

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

30 Naye akawajibu, “Hili ni jambo la kushangaza! Nyinyi hamjui ametoka wapi, lakini amenifumbua macho yangu!

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

30 Naye akawajibu, “Hili ni jambo la kushangaza! Nyinyi hamjui ametoka wapi, lakini amenifumbua macho yangu!

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

30 Yule mtu akawajibu, “Hili ni jambo la ajabu! Hamjui anakotoka, naye amenifungua macho yangu!

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

30 Yule mtu akawajibu, “Hili ni jambo la ajabu! Hamjui anakotoka, naye amenifungua macho yangu!

Tazama sura Nakili




Yohana 9:30
13 Marejeleo ya Msalaba  

vipofu wanapata kuona, viwete wanatembea, wenye ukoma wanatakasika, viziwi wanasikia, wafu wanafufuliwa, na maskini wanakhubiriwa khabari njema.


Yesu akawaambia, Hamkupata kusoma katika maandiko, Jiwe walilolikataa waashi, Hili lilikuwa jiwe kuu la pembeni; Neno hili limetoka kwa Bwana, Nalo ni ajabu machoni petu?


Akastaajahu kwa sababu ya kutokuamini kwao. Akazungukazunguka katika vile vijiji, akifundisha.


Akajibu, akawaambia, Enendeni, mkamweleze Yohana mliyoyaona na kuyasikia: vipofu wanapata kuona, viwete wanatembea, wenye ukoma wanatakasika, viziwi wanasikia, wafu wanafufuliwa, maskini wanakhubiriwa khahari njema:


Lakini ijapokuwa amefanya ishara kubwa namna hii mbele yao, hawakumwamini;


Yesu akajibu akamwambia, Je! Wewe u mwalimu katika Israeli, na haya huyafahamu?


Sisi twajua ya kuwa Mungu alisema na Musa, bali huyo hatujui atokako.


Twajua ya kuwa Mungu hawasikii wenye dhambi: bali mtu akiwa mcha Mungu, na kufanya mapenzi yake, huyo amsikia.


Kwa kuwa Mungu, aliyesema, Nuru itangʼaa toka gizani, ndive aliyengʼaa mioyoni mwetu, atupe nuru va elimu ya utukufu wa Mungu katika uso wa Yesu Kristo.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo