Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Yohana 9:16 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

16 Bassi baadhi ya Mafarisayo wakanena, Mtu huyu hakutoka kwa Mungu, kwa sababu haishiki sabato. Wengine wakanena, Awezaje mtu mwenye dhambi kufanya ishara kama hizo?

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

16 Baadhi ya Mafarisayo wakasema, “Mtu huyu hakutoka kwa Mungu, maana hashiki sheria ya Sabato.” Lakini wengine wakasema, “Mtu mwenye dhambi awezaje kufanya ishara za namna hii?” Kukawa na mafarakano kati yao.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

16 Baadhi ya Mafarisayo wakasema, “Mtu huyu hakutoka kwa Mungu, maana hashiki sheria ya Sabato.” Lakini wengine wakasema, “Mtu mwenye dhambi awezaje kufanya ishara za namna hii?” Kukawa na mafarakano kati yao.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

16 Baadhi ya Mafarisayo wakasema, “Mtu huyu hakutoka kwa Mungu, maana hashiki sheria ya Sabato.” Lakini wengine wakasema, “Mtu mwenye dhambi awezaje kufanya ishara za namna hii?” Kukawa na mafarakano kati yao.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

16 Baadhi ya Mafarisayo wakasema, “Huyu mtu hatoki kwa Mungu, kwa sababu hashiki Sabato.” Lakini wengine wakasema, “Awezaje mtu mwenye dhambi kufanya miujiza kama hii?” Wakagawanyika.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

16 Baadhi ya Mafarisayo wakasema, “Huyu mtu hatoki kwa Mungu, kwa sababu hashiki Sabato.” Lakini wengine wakasema, “Awezaje mtu mwenye dhambi kufanya miujiza kama hii?” Wakagawanyika.

Tazama sura Nakili

Yohana 9:16
18 Marejeleo ya Msalaba  

Na tazama mtu mwenye mkono umepooza, wakamwuliza, wakinena, Ni halali kuponya watu siku ya sabato? wapate kumshtaki.

Na Mafarisayo walipoona, wakamwambia, Tazama! wanafunzi wako wanatenda lililo haramu kutenda siku ya sabato.

Mkuu wa ile sunagogi akajibu, akiona hasira kwa sababu Yesu amemponya mtu siku ya sabato, akawaambia makutano, Kuna siku sita itupasapo kufauya kazi: katika hizo, bassi, njoni mponywe wala si katika siku ya sabato.

Yakaingia tena matangukano katika Wayahudi, kwa ajili ya maneno haya.

Niaminini ya kwamba mimi ni ndani ya Baba, na Baba ndani yangu; la! hamwamini hivyo, niaminini kwa sababu ya kazi zenyewe.

Kama singalitenda kazi kwao asizozitenda mtu mwingine, wasingalikuwa na dhambi; sasa wametuona mimi na Baba yangu, na kutuchukia.

Mwanzo huu wa ishara Yesu alifanya Kana ya Galilaya, akauonyesha utukufu wake, wanafunzi wake wakamwamini.

huyu alikuja kwa Yesu usiku, akamwambia, Rabbi, twajua ya kuwa u mwalimu, umetoka kwa Mungu; kwa maana hakuna mtu awezae kuzifanya ishara hizi uzifanyazo wewe, illa Mungu awe pamoja nae.

Kwa sababu hiyo Wayahudi wakamwambia yule aliyeponywa, Leo ni sabato, si halali kwako kujitwika kitanda chako.

Lakini ushuhuda nilio nao ni mkubwa kuliko ule wa Yohana: kwa kuwa zile kazi nilizopewa na Baba nizimalize, kazi hizo zenyeye ninazozitenda zinanishuhudia kwamba Baba amenituma.

Bassi Wayahudi wakashindana wao kwa wao, wakinena; Awezaje mtu huyu kutupa sisi nyama yake tuile?

Kukawa manungʼuniko mengi katika makutano kwa khabari zake; wengine wakisema, Yu mtu mwema; na wengine wakisema, Sivyo, bali anawadanganya makutano.

Bassi ikiwa mtu apashwa tohara siku ya sabato, torati ya Musa isije ikavunjika, mbona mnanikasirikia kwa sababu nalimfanya mtu kuwa mzima kabisa siku ya sabato?

Bassi yakaingia matangukano kwa ajili yake.

Bassi marra ya pili wakamwita yule mtu aliyekuwa kipofu wakamwambia, Mpe Mungu utukufu. Sisi tunajua ya kuwa mtu huyu ni mwenye dhambi.

Lakini jamii ya watu wa mjini wakagawanyikana: bawa walikuwa upande wa Wayahudi, na hawa upande wa Mitume.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo