Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yohana 8:52 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

52 Bassi Wayahudi wakamwambia, Sasa tumefahamu ya kuwa una pepo; Ibrahimu amekufa na manabii, na wewe wasema, Mtu akilishika neno langu, hataonja mauti kabisa hatta milele.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

52 Basi, Wayahudi wakasema, “Sasa tunajua kweli kwamba wewe una pepo! Abrahamu alikufa, na manabii pia walikufa, nawe wasema ati, ‘Anayeuzingatia ujumbe wangu hatakufa milele!’

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

52 Basi, Wayahudi wakasema, “Sasa tunajua kweli kwamba wewe una pepo! Abrahamu alikufa, na manabii pia walikufa, nawe wasema ati, ‘Anayeuzingatia ujumbe wangu hatakufa milele!’

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

52 Basi, Wayahudi wakasema, “Sasa tunajua kweli kwamba wewe una pepo! Abrahamu alikufa, na manabii pia walikufa, nawe wasema ati, ‘Anayeuzingatia ujumbe wangu hatakufa milele!’

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

52 Ndipo Wayahudi wakapaza sauti, wakamwambia, “Sasa tumejua kwamba una pepo mchafu! Ibrahimu alikufa, na manabii vilevile, nawe unasema kuwa mtu akitii neno lako hatakufa milele.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

52 Ndipo Wayahudi wakamwambia, “Sasa tumejua kwamba una pepo mchafu. Ikiwa Ibrahimu alikufa na vivyo hivyo manabii, nawe unasema, ‘Mtu akitii neno langu hatakufa milele.’

Tazama sura Nakili




Yohana 8:52
14 Marejeleo ya Msalaba  

Maana Yohana alikuja, hali wala hanywi, wakanena. Yuna pepo.


Na huu ndio ushuhuda wake Yohana, Wayahudi walipotuma makuhani na Walawi toka Yerusalemi wamwulize, Wewe u nani?


Yesu akajibu akamwambia, Mtu akinipenda, atalishika neno langu; na Baba yangu atampenda, nasi tutakuja kwake, na kufanya makao kwake.


Likumbukeni lile neno nililowaambieni, Mtumwa si mkubwa kuliko Bwana wake. Ikiwa waliniudhi mimi, watawaudhi ninyi nanyi: ikiwa walilishika neno langu, watalishika na lenu.


Jina lako nimewadhihirishia watu wale ulionipa katika ulimwengu; wahkuwa wako, ukanipa mimi: na neno lako wamelishika.


Makutano wakajibu, wakasema, Una pepo; ni nani anaetafuta kukuua?


Bassi Wayahudi wakanena, Je! atajiua, kwa kuwa anena, Niendako mimi hamwezi kuja?


Wayahudi wakajibu wakamwambia, Hatuneni vema sisi kwamba wewe u Msamaria, na una pepo?


Amin, amin, nawaambieni, Mtu akilishika neno langu, hataona mauti kabisa hatta milele.


Nanyi hamkumjua; lakini mimi namjua, na nikisema ya kwamba simjui, nitakuwa mwongo kama ninyi; lakini namjua na neno lake nalishika.


Bassi marra ya pili wakamwita yule mtu aliyekuwa kipofu wakamwambia, Mpe Mungu utukufu. Sisi tunajua ya kuwa mtu huyu ni mwenye dhambi.


Hawa wote wakafa katika imani, wasizipokee zile ahadi, bali wakiziona tokea mbali na kuzisalimu, na kukiri kwamba walikuwa wageni, na wasafiri juu ya inchi.


illa twamwona yeye aliyefanywa mdogo punde kuliko malaika, yaani Yesu, kwa sababu ya maumivu ya mauti, amevikwa taji ya utukufu na heshima, illi kwa neema ya Mungu aionje mauti kwa ajili ya killa mtu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo