Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yohana 8:51 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

51 Amin, amin, nawaambieni, Mtu akilishika neno langu, hataona mauti kabisa hatta milele.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

51 Kweli nawaambieni, anayeuzingatia ujumbe wangu hatakufa milele.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

51 Kweli nawaambieni, anayeuzingatia ujumbe wangu hatakufa milele.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

51 Kweli nawaambieni, anayeuzingatia ujumbe wangu hatakufa milele.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

51 Amin, amin nawaambia, mtu yeyote akilitii neno langu, hataona mauti milele.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

51 Amin, amin nawaambia, mtu yeyote akilitii neno langu hataona mauti milele.”

Tazama sura Nakili




Yohana 8:51
15 Marejeleo ya Msalaba  

Amin, nawaambieni, Pana watu katika hawo wanaosimama hapa, ambao hawataonja mauti kabisa, hatta watakapomwona Mwana wa Adamu akija katika ufalme wake.


Nae alikuwa amebashiriwa na Roho Mtakatifu ya kwamba haoni mauti kabla ya kumwona Kristo wa Bwana.


Yesu akajibu akamwambia, Mtu akinipenda, atalishika neno langu; na Baba yangu atampenda, nasi tutakuja kwake, na kufanya makao kwake.


Likumbukeni lile neno nililowaambieni, Mtumwa si mkubwa kuliko Bwana wake. Ikiwa waliniudhi mimi, watawaudhi ninyi nanyi: ikiwa walilishika neno langu, watalishika na lenu.


Jina lako nimewadhihirishia watu wale ulionipa katika ulimwengu; wahkuwa wako, ukanipa mimi: na neno lako wamelishika.


Amin, amin, nawaambieni, Alisikiae neno langu na kumwamini yeye aliyenipeleka ana uzima wa milele, wala hafiki hukumuni, bali amepita toka mauti hatta uzima.


Huu ni mkate ushukao kutoka mbinguni, illi mtu aule wala asife.


Bassi Yesu akanena nao tena, akisema. Mimi ni nuru ya ulimwengu; anifuatae hatakwenda katika giza kamwe, bali atakuwa na nuru ya uzima.


Bassi Wayahudi wakamwambia, Sasa tumefahamu ya kuwa una pepo; Ibrahimu amekufa na manabii, na wewe wasema, Mtu akilishika neno langu, hataonja mauti kabisa hatta milele.


Nanyi hamkumjua; lakini mimi namjua, na nikisema ya kwamba simjui, nitakuwa mwongo kama ninyi; lakini namjua na neno lake nalishika.


Kwa imani Enok alihamishwa, asije akaona mauti, wala hakuonekana, kwa sababu Mungu alimhamisha: maana kabla ya kuhamishwa kwake alikuwa ameshuhudiwa kwamba amempendeza Mungu.


illa twamwona yeye aliyefanywa mdogo punde kuliko malaika, yaani Yesu, kwa sababu ya maumivu ya mauti, amevikwa taji ya utukufu na heshima, illi kwa neema ya Mungu aionje mauti kwa ajili ya killa mtu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo