Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yohana 8:47 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

47 Aliye wa Mungu huyasikia maneno ya Mungu; kwa hiyo ninyi hamsikii, kwa sababu ninyi si wa Mungu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

47 Aliye wa Mungu husikiliza maneno ya Mungu. Lakini nyinyi hamsikilizi kwa sababu nyinyi si watu wa Mungu.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

47 Aliye wa Mungu husikiliza maneno ya Mungu. Lakini nyinyi hamsikilizi kwa sababu nyinyi si watu wa Mungu.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

47 Aliye wa Mungu husikiliza maneno ya Mungu. Lakini nyinyi hamsikilizi kwa sababu nyinyi si watu wa Mungu.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

47 Yeye atokaye kwa Mungu husikia kile Mungu asemacho. Sababu ya ninyi kutosikia ni kwa kuwa hamtokani na Mungu.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

47 Yeye atokaye kwa Mungu husikia kile Mungu asemacho. Sababu ya ninyi kutosikia ni kwa kuwa hamtokani na Mungu.”

Tazama sura Nakili




Yohana 8:47
17 Marejeleo ya Msalaba  

Anikataae mimi, asiyekubali maneno yangu, anae amhukumuye: neno lile nililolisema, ndilo litakalomhukumu siku ya mwisho.


Bassi Pilato akamwambia, Wewe u mfalme bassi? Yesu akajibu, Wewe wanena ya kwamba mimi ni mfalme. Mimi nalizaliwa kwa ajili ya haya na kwa ajili ya haya nalikuja ulimwenguni, illi niishuhudie kweli. Killa aliye wa kweli hunisikia sauti yangu.


Amin, amin, nawaambieni, Saa inakuja, na sasa ipo, wafu watakapoisikia sauti ya Mwana wa Mungu, na wale waisikiao watakuwa hayi.


Akanena, Kwa sababu hii nimewaambia ya kwamba hapana mtu awezae kuja kwangu, isipokuwa amejaliwa na Baba yangu.


Najua ya kuwa m mzao wa Ibrahimu; lakini mnatafuta kuniua kwa sababu neno langu halina nafasi ndani yenu.


Mbona hamyafahamu maneno yangu haya niyasemayo? Ni kwa sababu hamwezi kulisikia neno langu.


Nami, kwa sababu naisema kweli, hamniamini.


Hivi watoto wa Mungu ni dhahiri, na watoto wa Shetani. Mtu aliye yote asiyefanya haki hatokani na Mungu, wala yeye asiyempenda ndugu yake.


KILLA mtu aaminiye kwamba Yesu ni Kristo amezaliwa na Mungu. Na killa mtu ampendae mwenye kuzaa ampenda na yeye mwenye kuzaliwa nae.


Killa aendeleae mbele, asidumu katika ma-fundisho ya Kristo, hana Mungu. Yeye adumuye katika mafundisho ya Kristo, mtu huyu ana Baba na Mwana pia.


Mpenzi, usiuige ubaya, bali wema. Yeye atendae mema ni wa Mungu, bali yeye atendae mabaya hakumwona Mungu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo