Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yohana 8:42 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

42 Yesu akawaambia, Kama Mungu angekuwa baba yenu mngenipenda mimi; kwa maana nalitoka kwa Mungu, na nimekuja; wala sikuja kwa nafsi yangu, bali yeye ndiye aliyenituma.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

42 Yesu akawaambia, “Kama Mungu angekuwa Baba yenu, mngenipenda mimi, maana mimi nilitoka kwa Mungu na sasa niko hapa. Sikuja kwa mamlaka yangu mwenyewe, ila yeye alinituma.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

42 Yesu akawaambia, “Kama Mungu angekuwa Baba yenu, mngenipenda mimi, maana mimi nilitoka kwa Mungu na sasa niko hapa. Sikuja kwa mamlaka yangu mwenyewe, ila yeye alinituma.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

42 Yesu akawaambia, “Kama Mungu angekuwa Baba yenu, mngenipenda mimi, maana mimi nilitoka kwa Mungu na sasa niko hapa. Sikuja kwa mamlaka yangu mwenyewe, ila yeye alinituma.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

42 Isa akawaambia, “Kama Mungu angekuwa Baba yenu, mngenipenda, kwa maana nilitoka kwa Mungu na sasa niko hapa. Sikuja kwa ajili yangu mwenyewe, ila yeye alinituma.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

42 Isa akawaambia, “Kama Mungu angekuwa Baba yenu, mngenipenda, kwa maana nilitoka kwa Mungu na sasa niko hapa. Sikuja kwa ajili yangu mwenyewe, ila yeye alinituma.

Tazama sura Nakili




Yohana 8:42
22 Marejeleo ya Msalaba  

Nae Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu, tukautazama utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee akitoka kwa Baba, amejaa neema na kweli.


Kwa maana mimi sikusema kwa nafsi yangu tu; bali yeye aliyenipeleka, yaani Baba, ameniagiza nitakayonena na nitakayosema.


bassi Yesu akijua ya kuwa Baba amempa vyote mikononi mwake, na ya kuwa alitoka kwa Mungu, na anakwenda kwa Mungu,


Huamini ya kwamba mimi ni ndani ya Baba, na Baba ndani yangu? Maneno niwaambiayo mimi, sisemi kwa shauri langu tu; lakini Baba akaae ndani yangu huzifanya kazi zake.


Sasa tumejua ya kuwa unajua yote, wala huhitaji mtu akuulize; kwa hiyo twaamini ya kwamba ulitoka kwa Mungu.


Baba mwenye haki, ulimwengu haukukujua, lakini mimi nalikujua; na hawa walijua ya kuwa ndiwe uliyenituma.


kwa kuwa maneno uliyonipa nimewapa wao; wakavapokea, wakajua hakika ya kuwa nalitoka kwako, wakaamini ya kwamba ndiwe uliyenituma.


Maana Mungu hakumpeleka Mwana wake ulimwenguni auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe nae.


illi wote wamheshimu Mwana kama wanavyomheshimu Baba. Asiyemheshimu Mwana, hamheshimu Baba aliyempeleka.


Mimi nimekuja kwa jina la Baba yangu, nanyi hamnipokei: mwingine akija kwa jina lake mwenyewe mtampokea huyo.


Yesu akajibu akawaambia, Ningawa mimi ninajishuhudia nafsi yangu, ushuhuda wangu ni kweli, kwa sababu najua nilikotoka na niendako; lakini ninyi hamjui nilikotoka, wala niendako.


Mtu aliye yote asiyempenda Bwana Yesu Kristo, na awe anathema. Maranatha.


Hatta ulipowadia utimilifu wa wakati, Mungu alimtuma Mwana wake, amezaliwa na mwanamke, amezaliwa chini ya sharia,


Na sisi tumeona na kushuhudu ya kuwa Baba amempeleka Mwana kuwa Mwokozi wa ulimwengu.


Twajua kwamba Mwana wa Mungu amekwisha kuja, nae ametupa akili illi tumjue yeye aliye wa kweli, nasi tumo ndani yake yeye aliye wa kweli, ndani ya Mwana wake Yesu Kristo. Huyu ndiye aliye Mungu wa kweli na uzima wa milele.


AKANIONYESHA mto wa maji ya uzima, wenye kungʼaa kama bilauri, ukitoka katika kiti cha enzi cha Mungu, na cha Mwana kondoo.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo