Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yohana 8:37 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

37 Najua ya kuwa m mzao wa Ibrahimu; lakini mnatafuta kuniua kwa sababu neno langu halina nafasi ndani yenu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

37 Najua kwamba nyinyi ni wazawa wa Abrahamu. Hata hivyo, mnataka kuniua kwa sababu hamyakubali mafundisho yangu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

37 Najua kwamba nyinyi ni wazawa wa Abrahamu. Hata hivyo, mnataka kuniua kwa sababu hamyakubali mafundisho yangu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

37 Najua kwamba nyinyi ni wazawa wa Abrahamu. Hata hivyo, mnataka kuniua kwa sababu hamyakubali mafundisho yangu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

37 Ninajua ya kuwa ninyi ni wazao wa Ibrahimu, lakini mnatafuta wasaa wa kuniua kwa sababu ndani yenu hamna nafasi ya neno langu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

37 Ninajua ya kuwa ninyi ni wazao wa Ibrahimu, lakini mnatafuta wasaa wa kuniua kwa sababu ndani yenu hamna nafasi ya neno langu.

Tazama sura Nakili




Yohana 8:37
22 Marejeleo ya Msalaba  

Maana moyo wa watu hawa umekuwa mzito, Na kwa masikio yao hawasikii vema, Na macho yao wameyafumba; Wasije wakaona kwa macho yao Wakasikia kwa masikio yao, Wakafahama kwa mioyo yao, Wakaongoka, Nikawaponya.


msiwaze moyoni kwamba, Tuna baba, ndiye Ibrahimu; kwa maana nawaambieni ya kwamba Mungu anaweza katika mawe haya kumwinulia Ibrahimu watoto.


Bassi Wayahudi wakaokota mawe tena, illi wampige.


Bassi tangu siku ile walifanya shauri wapate kumwua.


Mwawezaje kuamini ninyi mnaopokezanya utukufu ninyi kwa ninyi, na utukufu ule utokao kwa Mungu aliye wa pekee hamwutafuti?


NA baada ya haya Yesu akawa akitembea katika Galilaya: maana hakutaka kutembea katika Yahudi, kwa sababu Wayahudi walikuwa wakitafuta kumwua.


Aliyewapeni torati si Musa? wala hapana mmoja wenu aitendae torati. Mbona mnatafuta kuniua?


Bassi baadhi ya watu wa Yerusalemi wakanena, Huyu si yeye wanaemtafuta illi kumwua?


Wakamjihu, Tu uzao wake Ibrahimu, wala hatujawa watumwa wa mtu wakati wo wote; nawe wanenaje, Mtawekwa huru?


Mbona hamyafahamu maneno yangu haya niyasemayo? Ni kwa sababu hamwezi kulisikia neno langu.


Ibrahimu baba yemi alishangilia apate kuiona siku yangu; akaona, akafurahi.


Bassi wakatwaa mawe wamtupie; lakini Yesu akajificha, akatoka hekaluni.


Wakasema neno hili wakimjaribu wapate sababu ya kumshitaki. Lakini Yesu akainama, akaandika kwa kidole chake katika inchi.


Ndugu zangu, wana wa ukoo wa Ibrahimu, nao miongoni mwenu mnaomcha Mungu, kwenu ninyi neno la wokofu huu limepelekwa.


Wala hawawi wote wana kwa kuwa wazao wa Ibrahimu, bali, Katika Isaak wazao wako watakwitwa;


Bassi mwana Adamu wa tabia ya asili hayapokei mambo ya Mungu; maana kwake huyu ni mapumbavu, wala hawezi kuyajua, kwa kuwa yatambulikana kwa jinsi ya rohoni.


Nimewaandikia ninyi, akina baba, kwa sababu mmemjua yeye aliye tangu mwanzo. Nimewaandikia ninyi, vijana, kwa sababu m hodari, na neno la Mungu linakaa ndani yenu, na mmemshinda yule mwovu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo