Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yohana 8:31 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

31 Bassi Yesu akawaamhia Wayahudi wale waliomwamini, Ninyi mkikaa katika neno langu, mu wanafunzi wangu kweli kweli;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

31 Basi, Yesu akawaambia wale Wayahudi waliomwamini, “Kama mkiyazingatia mafundisho yangu mtakuwa kweli wanafunzi wangu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

31 Basi, Yesu akawaambia wale Wayahudi waliomwamini, “Kama mkiyazingatia mafundisho yangu mtakuwa kweli wanafunzi wangu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

31 Basi, Yesu akawaambia wale Wayahudi waliomwamini, “Kama mkiyazingatia mafundisho yangu mtakuwa kweli wanafunzi wangu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

31 Kisha Isa akawaambia wale Wayahudi waliomwamini, “Mkidumu katika maneno yangu, mtakuwa wanafunzi wangu kweli kweli.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

31 Kisha Isa akawaambia wale Wayahudi waliomwamini, “Kama mkidumu katika maneno yangu, mtakuwa wanafunzi wangu kweli kweli.

Tazama sura Nakili




Yohana 8:31
25 Marejeleo ya Msalaba  

Lakini astahimiliye hatta mwisho, ndiye atakaeokoka.


Yesu akamwona Nathanaeli akija kwake, akamtaja khabari zake, Tazama, huyu ni Mwisraeli kweli kweli, hamna hila ndani yake.


Yesu nae akaitwa pamoja na wanafunzi wake arusini.


Kwa maima nyama yangu ni chakula cha kweli, na damu yangu ni kinywaji cha kweli,


Bassi Mwana akiwaweka huru mtakuwa huru kweli kweli.


Sunagogi lilipofumukana, Wayahudi wengi na waongofu watawa wakashikamana na Paolo na Barnaba; nao, wakisema nao, wakawatia moyo kudumu katika neema ya Mungu.


wakifanya imara roho za wanafunzi na kuwaonya wakae katika imani, na ya kwamba imetupasa kuingia katika ufalme wa Mungu kwa njia ya shidda nyingi.


Bassi nikiisha kuupata msaada utokao kwa Mungu nimesimama hatta leo hivi nikiwashuhudia wadogo kwa wakubwa, wala sisemi neno illa yale ambayo manabii na Musa waliyasema, kwamba yatakuwa;


Fahamu, bassi, wema na ukali wa Mungu; kwa wale walioanguka ukali, bali kwako wema, ukikaa katika wema huo; kama sivyo, wewe nawe utakatiliwa mbali.


wale ambao kwa kustahimili katika kutenda mema wanatafuta utukufu na heshima na kutoa kuharibika, nzima wa milele;


mkidumu tu katika imani, mmewekwa juu ya misingi, mkawa imara; msipogeuzwa na kuliacha tumaini la Injili mliyosikia khabari zake, iliyokhubiriwa katika viumbe vyote vilivyo chini ya mbingu; ambayo mimi Paolo nalikuwa mkhudumu wake.


Lakini ataokolewa, kwa ule uzazi, kama wakidumu katika imani na npendo na utakatifu pamoja na moyo wa kiasi.


Jitunze nafsi yako, na yale mafundisho. Ukadumu katika hayo; maana kwa kufanya hivi utajiokoa nafsi yako nao wakusikiao.


Bali wewe ukae katika yale uliyofundishwa na kuhakikishwa, kwa maana unajua ni nani ambae ulijifunza kwake,


Kwa maana tumekuwa washirika wa Kristo, kama tukishikamana na mwanzo wa uthabiti wetu mpaka mwisho;


Kwa sababu hawakudumu katika agano langu, mimi nami sikuwaangalia, asema Bwana.


Lakini aliyeitazama sharia kamilifu ya uhuru, na kukaa humo, asiwe msikiaji msahaulifu, bali mtendaji wa kazi, huyu atakuwa wa kheri katika kutenda kwake.


Walitoka kwetu, bali hawukuwa wa kwetu. Maana kama wangalikuwa wa kwetu, wangalikaa pamoja nasi. Lakini walitoka illi wafunuliwe kwamba si wote walio wa kwetu.


Bassi, na yakae ndani yenu maneno yale mliyoyasikia tangu mwanzo. Neno lile mlilolisikia tangu mwanzo likikaa ndani yenu, ninyi nanyi mtakaa ndani ya Mwana, na ndani ya Baba.


Killa aendeleae mbele, asidumu katika ma-fundisho ya Kristo, hana Mungu. Yeye adumuye katika mafundisho ya Kristo, mtu huyu ana Baba na Mwana pia.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo